35 kupigania fursa ya kucheza dhidi ya Bandari FC

35 kupigania fursa ya kucheza dhidi ya Bandari FC

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

WACHEZAJI 35 kutoka klabu mbalimbali watapigania fursa ya kuwa miongoni mwa wachezaji 23 watakaounda kikosi cha Lamu Combined kitakachocheza na Bandari FC na Bandari Youth.

Kikosi cha wanasoka hao 35 kilichotangazwa na Mwenyekiti wa tawi la Kaunti ya Lamu la Shirikisho la Soka la Kenya (FKF), Fuad Ali Adi na katibu wake Mohamed Athman, kinatarajia kufanya mazoezi kupunguza idadi ya wachezaji hadi kufikia 23.

“Tunashukuru afisi ya Halmashauri ya Bandari za Kenya (KPA) kutukubalia kuidhamini timu ya Lamu Combined kufanya ziara ya mechi mbili dhidi ya timu ya ligi kuu ya Bandari FC na timu ya Bandari Youth inayoshiriki ligi ya FKF ya Mombasa,” akasema Athman.

Adi ameambia Taifa Leo Dijitali kuwa wachezaji hao 35 watafanya mazoezi chini ya wakufunzi watakaowataja ili kutafuta wanasoka bora 23 watakaosafiri hadi Mombasa kucheza na timu hizo mbili za Bandari.

Wanasoka hao 35 ni Balan Jabir, Abdulfatah Mohamed, Kassim Mohamed, Mohamed Suleiman, Abdul Shukri, Issa Islam, Athman Osman, Ahmed Abbas, Mohamed Ahmed, Abdulhalim Mohamed, Abu Salim, Bwana Ali, Noor Issa, Nurein Imam, Nuhu Adu na Musa Killa.

Wengine ni Francis Wambua, Mohamed Fuad, Kauthar Abdul, Salim Ali, Ibrahim Ahmed, Francis Mburu, Peter Mwema, Jaffar Swaleh, Yusuf Shora, Ghalib Aziz, Sultan Omar, Hassan Harun, Titus Shume, Shukran Katona, Titus Wekesa , Swaleh Fuad, Adam Abdalla, Hassan Nuh na Barack Okoth

Athman amesema wanatarajia ziara hiyo itakuwa ya mafanikio makubwa hasa kwa wachezaji ambao wataonekana na wale wenye vipaji huenda wakavutia maafisa wa klabu hizo mbili kuwasajili kwa msimu mpya.

  • Tags

You can share this post!

Lempurkel akana shtaka la kueneza chuki Laikipia

TAHARIRI: Ahadi ya kazi kwa vijana iko wapi?