Habari Mseto

Ashangaza kumuua babaye mzazi

July 6th, 2020 1 min read

NICHOLAS KOMU na FAUSTINE NGILA

Mwanamume amemuua babaye  wa miaka 84 eneo la Tetu, Kaunti ya Nyeri kufuatia mzozo wa nyumbani.

Bw Kiragu Wambugu anayesemekana kuwa wa miaka thelathini alimvamia babake kwa panga Joseph Wambugu Jumapili asubuhi kufuatia mzozo ulioanza Jumamosi usiku.

Kulingana na jamaa zao, wawili hao wamekuwa na mgogoro wa miaka mingi uliozua vita.

Bw Boniface Ndugo, nduguye mwendazake aliiambia Taifa Leo kwamba mgogoro wa nduguye na mwanawe ulikuwa umefika kiwango hatari.

“Wamekuwa wakizozana kwa muda mrefu. Usiku wa jana waligombana na kijana huyo akaamkia kumkata babake kwa panga,” alisema Bw Ndugo.

Baada ya kuvamiwa, mzee huyo alikimbizwa hospitali ambapo alikata roho kwa maumivu.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Nyeri Aiel Nyage alithibitisha hayo mshukiwa alikamatwa na atafikisha kortini Jumatatu.

Tukio hilo lilijiri wakati polisi wanang’ang’ana kujua kiini cha mauaji ya kinyumbani na ya kujiua yalioripotiwa katika Kijiji cha Kiamwathi mji wa Nyeri wiki iliyopita.

Wanawake wawili walikatwa hadi kifo ilioripotiwa na mwanaume aliyejiua nyumbani kwa mwajiri wake.

Ilitambulika kwamba mwanamke mmoja aliuwawa kwa kutumia panga yukio ambalo linakisiwa kuwa shambulizi.