57 kuosha jiji kwa kukiuka kanuni za Covid

57 kuosha jiji kwa kukiuka kanuni za Covid

Na COLLINS OMULO

WAZUNGU na Wachina wanne ni miongoni mwa watu 57 waliolazimika kusafisha sehemu za jiji la Nairobi, baada ya kupatikana na hatia ya kukiuka masharti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hilo linafuatia juhudi mpya zinazoendeshwa na serikali ya kitaifa dhidi ya Wakenya wanaovunja kanuni hizo zilizowekwa na Wizara ya Afya.

Masharti hayo ni watu kutokusanyika kwenye makundi makubwa, kuvaa barakoa na kuosha mikono.

Watu hao, ambao walikamatwa katika eneo moja la burudani, walizuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani, ambapo baadaye walifikishwa katika Mahakama ya Kibera mnamo Jumatatu.

Baada ya hapo, walikabidhiwa kwa Halmashauri ya Huduma za Jiji (NMS) ili kutekeleza adhabu ya kuihudumia jamii.

Washtakiwa walikuwa wakishiriki burudani katika kilabu cha Onyx Lounge.

Baadhi yao walipatikana wakinywa pombe nje ya muda uliowekwa kuhusu kafyu huku wengine wakipatikana bila barakoa. Baadhi hawakuwa wakizingatia sharti la kutokaribiana.

Kulikuwa na ripoti kwamba Wazungu na Wachina waliokamatwa ni watalii, lakini polisi wakapuulizia mbali ripoti hizo.

Kamanda wa polisi katika kaunti ndogo ya Kilimani, Bw Vitalis Otieno, alisema watu hao wote ni Wakenya.

  • Tags

You can share this post!

Wageni kutoka Tanzania kuwekwa karantini Mombasa

Raila, Uhuru waamua kupimana nguvu Kisii