Habari Mseto

61 waliosafiri kinyume cha sheria wawekwa karantini kwa gharama yao

June 17th, 2020 1 min read

MANASE OTSIALO

Polisi wa kaunti ya Mandera wamekamata dereva aliyesafirisha watu 61 kutoka mji wa Nairobi kinyume na makataa ya kutotoka au kuingia Nairobi.

Rais Uhuru Kenyatta alizima kuingia au kutoka kaunti za Nairobi, Mombasa na Mandera ambapo visa vingi vya corona vimeripotiwa.

Alhamisi Gavana wa Kaunti ya Mandera aliagiza kufungwa kwa kaunti hiyo kufuatia maambukizi zaidi huku watu wawili wakithibitishwa kuwa na virusi hivyo na wengine 30 waliotangamana na wawili haokutengwa.

Mshirikishi wa kaunti hiyo Onesmus Kyatha alisema kwamba basi hilo la Makka lilishikwa katika mji wa Elwak Mandera Kusini baada ya kufika saa mbili usiku.

Wtu hao 61 waliwasili kwa gari hilo wamewekwa kwenye karantini Elwak kwa siku 14 kwa gharama zao.

“Dereva huyo tumemzuilia anayekisiwa kusafirisha watu hao kutoka Nairobi kinyume na amri ya serikali tutamshtaki,” alisema Bw Kytha.

Hayo yanajiri baada ya Gavana Roba kutaja kwamba usafiri kati ya Nairobi na Mandera ulikuwa unaendelea…

Bw Kyatha alisema waliweza kuwashika asilimia 90 ya waaliowasili Mandera Aprili 1 na wako karantini wakisubiri kupimwa.