• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
iHub yazindua vituo vya uvumbuzi Marsabit na Garissa kuokoa jamii

iHub yazindua vituo vya uvumbuzi Marsabit na Garissa kuokoa jamii

Na BERNARDINE MUTANU

KAMPUNI ya uvumbuzi ya iHub imezindua vituo Marsabit na Garissa kwa lengo la kuwasaidia wakazi wa eneo hilo walioathiriwa na ukame.

Vituo hivyo vitaendeshwa kwa miezi 21 kwa ufadhili wa UK Aid.

iHub inashirikiana na Mastercard International na Adeso, shirika la kutoa msaada wa kibinadamu iliyo na makao yake Nairobi.

Kampuni hiyo inalenga kuisaidia jamii maeneo hayo kupata suluhu kwa matatizo yao badala ya kutegemea watu kutoka nje.

Wavumbuzi watapewa nafasi ya kufanyia majaribio dhana zao na kupokea utathmini kutoka kwa wataalamu.

You can share this post!

Riba ya ‘Okoa Jahazi’ ya Safaricom ni haramu,...

Kuchelewa kwa mvua kutaibua baa la njaa nchini

adminleo