• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 5:29 PM
Chiloba sasa apata kazi serikalini baada ya kutimuliwa na IEBC

Chiloba sasa apata kazi serikalini baada ya kutimuliwa na IEBC

Na VALENTINE OBARA

ALIYEKUWA Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Bw Ezra Chiloba, atafungua mwaka kwa hali nafuu baada ya serikali kumkumbuka kwa ajira.

Waziri wa Habari na Mawasiliano, Bw Joe Mucheru, Alhamisi alimwajiri Bw Chiloba kuwa mmoja wa wanachama wa bodi ya Hazina ya Kustawisha Uwekezaji wa Vijana kwa miaka mitatu.

Tangazo hilo lilichapishwa kwenye gazeti rasmi la serikali.

Bw Chiloba alisimamishwa kazi mwaka wa 2018, pale Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati aliposema alihusika katika ukiukaji wa sheria za ununuzi wa bidhaa za umma.

Wakati huo huo, serikali imeongeza muda wa kuhudumu kwa Baraza la viongozi wa dini wanaoshughulikia masuala ya janga la corona.

Katika chapisho hilo la gazeti la serikali, Waziri wa Usalama wa Nchi, Dkt Fred Matiang’i alisema baraza hilo limeongezwa miezi sita kuanzia Januari 1.

Baraza hilo linaloongozwa na Askofu Mkuu Anthony Muheria wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Nyeri, hushughulikia zaidi utoaji mwongozo kuhusu mbinu za ibada wakati wa janga la corona.

You can share this post!

Pwani walisota zaidi Kenya 2020 – Utafiti

MAWAIDHA YA KIISLAMU: Husuda ni donda linalotoneshwa na...