• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 6:55 AM
Wito shule ziajiri walinzi wenye tajriba kuhakikisha usalama kipindi cha Covid

Wito shule ziajiri walinzi wenye tajriba kuhakikisha usalama kipindi cha Covid

Na TITUS OMINDE

SHULE zote kote nchini zimetakiwa kukodisha huduma za walinzi wa kibinafsi kutoka kwa kampuni za usalama zilizosajiliwa, ili kuhakikisha usalama wa watoto shuleni kipindi hiki cha janga la Covid-19.

Chama cha walinzi binafsi kimeonya shule dhidi ya kuajiri wazee ambao hawana mafunzo rasmi katika masuala ya usalama.

Mwenyekiti wa Chama cha walinzi wakibinafsi North Rift, Bw Peter Odima, alisema shule nyingi zinaajiri watu wasiofahamu masuala ya usalama na afya.

“Tunatoa wito kwa wizara ya elimu na afya kuhakikisha kwamba shule zinaajiri walinzi kutoka kampuni za usalama zinazojulikana kuwa na mafunzo sahihi katika masuala ya usalama,” akasema Bw Odima.

Akiongea mjini Eldoret, Bw Odima alisema ni kinyume cha sheria kuajiri walinzi wasiotoka kwa kampuni za usalama zinazotambuliwa kisheria.

“Tumeona visa vya walinzi wasiotoka kampuni zilizosajiliwa, wakifanya uhalifu shuleni na kutoweka wasipatikane waliko. Ni muhimu kwa shule kuajiri walinzi kutoka kwa kampuni ambazo zitawajibika iwapo,” akasema.

Karibu miaka miwili iliyopita wizara ya Mambo ya Ndani ilizindua mwongozo mpya wa mafunzo kwa maafisa wa usalama zaidi ya 700,000 ambao ulisimamiwa na waziri Fred Matiang’i.

Wakati wa mafunzo hayo Bw Matiang’i alisema mtaala huo ni sehemu ya mahitaji ya Sheria ya Kanuni za Usalama za Kibinafsi za mwaka wa 2016, ambapo kila kiila mtoa huduma ya usalama kibinafsi anapaswa kupokea mafunzo hayo ambayo yaliyothibitishwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usalama kibinafsi (PSRA).

Mafunzo hayo husaidia walinzi kuwa na ufahamu kuhusu masuala ya usalama na ulinzi wakati wa mashambulio kazini kwao.

Pia huwapa walinzi ujuzi wa kimsingi juu ya jinsi ya kukabiliana na shughuli za ugaidi mahali pao pa kazi.

  • Tags

You can share this post!

Wakazi sasa wataka daraja liwekwe kivuli kuzuia jua

SHULE: Wadau muhimu ngazi zote za serikali waelezea...