• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Madereva kupimwa ulevi, safari za treni kuongezwa

Madereva kupimwa ulevi, safari za treni kuongezwa

Na CHARLES WASONGA

MADEREVA wa matatu na magari mengine watapimwa ulevi kuanzia leo kama sehemu ya mikakati ya kupunguza visa vya ajali za barabarani shule zinapofunguliwa baada ya kufungwa kwa kipindi kirefu kufuatia mlipuko wa Covid-19.

Hii ni mojawapo ya mikakati iliyotangazwa jana na serikali kwa ajili ya kulainisha uchukuzi wa umma kuhakikisha usalama wa wanafunzi na wazazi wanaposafiri kuelekea shuleni

Waziri wa Uchukuzi James Macharia pia alitangaza idadi ya treni za SGR kati ya Nairobi na Mombasa zitaongezwa kuanzia leo.

“Kuanzia kesho (leo Jumatatu) kutakuwa na treni mbili za abiria kutoka Nairobi hadi Mombasa ambazo zitakuwa zikisimama katika vituo vyote saba katika ruti hiyo. Kwa upande mwingine, treni mbili kutoka Mombasa hadi Nairobi zitasimama katika vituo vyote kuhakikisha wanafunzi na wazazi wao wanafika shuleni kwa wakati,” akasema.

Bw Macharia ambaye alikuwa akiongea na wanahabari katika nje ya jumba la KICC aliongeza kuwa treni kutoka Nairobi hadi Nanyuki nayo itasafirisha zaidi ya abiria 1,500 na itasimama katika vituo vyote katika ruti hiyo inayoelekea Kati mwa Kenya.

Bw Macharia aliandamana na mawaziri wengine wakiongozwa na mwenzake wa Usalama wa Ndani Fred Matiang’i kutoa taarifa kuhusu ufunguzi wa shule.

Waziri huyo wa uchukuzi aliongeza kuwa wizara yake imekubaliana na Chama cha Wamiliki wa Matatu (MOA) kwamba madereva wote wapimwe ulevi ili kupunguza visa vya ajali.

“Tumefikiana kuhusu hatua kama hii kwa sababu ajali nyingi za barabarani hushuhudiwa wakati kama huu. Aliwaomba wahudumu wa matatu kutoongeza nauli.

  • Tags

You can share this post!

Baadhi ya watumiaji mitandao ya kijamii wakosoa Uhuru...

Mgao wa masomo kufika shule wiki hii