• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:58 PM
Nairobi: Mutura afanya mabadiliko kiasi katika serikali yake

Nairobi: Mutura afanya mabadiliko kiasi katika serikali yake

Na CHARLES WASONGA

KAIMU Gavana wa Kaunti ya Nairobi Benson Mutura amefanya mabadiliko kiasi katika serikali yake.

Aliyekuwa Waziri wa Elimu katika kaunti Janet Ouko amerejeshwa katika wadhifa uo huo. Bi Ouko alijiuzulu mnamo Julai 2019 baada ya kutofautiana na aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Sonko.

Naye Waziri wa Elimu wa hivi punde Lucia Mulwa amekabidhiwa mikoba ya ile ya Kilimo.

Wengine katika baraza hilo la mawaziri wa kaunti ni Jairus Musumba ambaye amepewa wadhifa wa Kaimu Katibu wa Kaunti, mwanaharakati Brian Weke ambaye ni mshauri wa masuala ya kisheria katika ofisi ya gavana, na Paul Mutungi ambaye atakuwa Mkuu wa Wafanyakazi.

Bw Weke ni mwanasiasa ambaye amewahi kuwania wadhifa wa ubunge wa Kamukunji, Nairobi.

“Nimefanya mabadilko haya kwa mujibu wa mamlaka ambayo imepewa afisi ya gavana wa Nairobi na Katiba ya Kenya na Sheria ya Serikali za Kaunti, 2012 na kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa serikali ya Kaunti ya Nairobi,” akasema Bw Mutura kwenye taarifa kuhusu mabadiliko hayo.

You can share this post!

ULIMBWENDE: Ndizi na urembo

GWIJI WA WIKI: Hussein Kassim