• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Kikosi cha Apoel champiga kalamu kocha Mick McCarthy baada ya miezi miwili pekee

Kikosi cha Apoel champiga kalamu kocha Mick McCarthy baada ya miezi miwili pekee

Na MASHIRIKA

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Ireland, Mick McCarthy amelazimika kuacha kukitumikia kikosi cha Apoel kinachoshiriki Ligi Kuu ya Cyprus miezi miwili pekee baada ya kupokezwa mikoba ya ukufunzi.

McCarthy, 61, aliajiriwa na Apoel mnamo Novemba 2 kwa pamoja na Terry Connor aliyekuwa msaidizi wake kambini mwa Wolves, Ipswich FC na timu ya taifa ya Jamhuri ya Ireland hapo awali.

Hata hivyo, Apoel walisajili ushindi katika mechi mbili pekee kati ya nane alizozisimamia huku kikosi kikipoteza mechi nne zilizopita mfululizo na kushuka hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa jedwali la Ligi Kuu.

“Tumekatiza rasmi uhusiano wetu na McCarthy pamoja na aliyekuwa msaidizi wake Connor. Tunawatakia kila la heri katika vibarua vyao vya baadaye kwingineko,” ikasema sehemu ya taarifa iliyotolewa na Apoel.

Baada ya Apoel kuajiri McCarthy, nafasi yake katika timu ya taifa ya Ireland ilitwaliwa na Stephen Kenny.

Apoel kwa sasa wamejivunia huduma za wakufunzi 13 tofauti tangu mwaka wa 2015.

  • Tags

You can share this post!

KNPC yataja kikosi cha Riadha za Walemavu za Dubai Para...

Kenya Prisons na KCB waanza kujinoa kwa Ligi Kuu ya...