• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 11:16 AM
Kenya Prisons na KCB waanza kujinoa kwa Ligi Kuu ya Voliboli ya Wanawake msimu huu wa 2021

Kenya Prisons na KCB waanza kujinoa kwa Ligi Kuu ya Voliboli ya Wanawake msimu huu wa 2021

Na CHRIS ADUNGO

VIKOSI vya Kenya Prisons na KCB vimeanza kujiandaa kwa kampeni za msimu ujao wa 2020-21 katika Ligi Kuu ya Voliboli ya Wanawake ambao utafunguliwa rasmi mnamo Januari 23.

Prisons wanaojifua katika uwanja wa Nairobi West hata hivyo watalazimika kushiriki kivumbi cha muhula huu bila huduma za nyota Loice Jepkosgei ambaye yuko katika likizo ya uzazi.

Kwa mujibu wa ratiba mpya ya Shirikisho la Voliboli la Kenya (KVF), Prisons wameratibiwa kufungua kampeni zao dhidi ya Kenya Army kabla ya kupepetana na wanabenki wa KCB.

Kwa mujibu wa Azenga Mavisi ambaye ni kocha msaidizi wa Prisons, vipusa wake kwa sasa wanashiriki vipindi vingi vya mazoezi ya viungo vya mwili na uthabiti wa akili.

“Mechi mbili za ufunguzi wa msimu zitakuwa kibarua kizito cha Prisons. Lakini tumejiandaa vya kutosha na tutakuwa na kila sababu ya kuibuka washindi ikizingatiwa ukubwa wa kiwango cha mazoezi tunayoyafanya,” akasema Mavisi.

Kukosekana kwa Jepkosgei, kunatarajiwa kuwapisha wachezaji Lydia Maiyo, Emmaculate Chemutai na Yvonne Wavinya kuunga kikosi cha kwanza cha Prisons.

Matarajio pia ni mengi kwa upande wa KCB ambao wamejinasia huduma za wanasoka matata kutoka kambi za Kenya Prisons na Kenya Pipeline. Mercy Moim na Edith Wisa waliosajiliwa kutoka Prisons ni miongoni mwa wachezaji waliojiunga rasmi na KCB ya kocha Japhet Munala muhula huu.

KCB ambao wamepangiwa kufungua kampeni zao dhidi ya kikosi cha Idara ya Upepelezi ya keshi za jinai (DCI) katika siku ya kwanza, wanajivunia pia huduma za Sharon Chepchumba aliyesajiliwa kutoka kambini mwa Oilers.

KCB kwa sasa wanafanya mazoezi yao katika uwanja wa Nairobi KCB Sports Club, Ruaraka watakaokuwa wakitumia kwa minajili ya michuano yao ya nyumbani.

  • Tags

You can share this post!

Kikosi cha Apoel champiga kalamu kocha Mick McCarthy baada...

AK kutumia mchujo wa kitaifa mnamo Julai ugani Kasarani...