• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Ruto ashauriwa kuungana na Kalonzo kupenya Ukambani

Ruto ashauriwa kuungana na Kalonzo kupenya Ukambani

NA WANDERI KAMAU

NAIBU Rais William Ruto ameshauriwa kuwa kuungana na kiongozi wa Wiper, Bw Kalonzo Musyoka, ndiyo njia pekee ambapo atapata uungwaji mkono kutoka eneo la Ukambani.

Kauli hiyo ilitolewa na Seneta Mutula Kilonzo Junior wa Makueni Jumamosi, kwenye hafla ya mazishi ya mjombake, Bw James Ngui, katika kijiji cha Ngaani, Kaunti Ndogo ya Mbooni, Kaunti ya Makueni.

Bw Kilonzo alitoa kauli hiyo baada ya aliyekuwa Seneta wa Machakos, Bw Johnstone Muthama, kumtaka Bw Kilonzo kumrai Bw Musyoka “kukoma kuipoteza kisiasa jamii ya Akamba.”

Bw Musyoka amekuwa akiunga mkono handisheki kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, huku Bw Muthama akiwa miongoni mwa viongozi kutoka eneo hilo wanaomuunga mkono Dkt Ruto

.“Ndugu yangu Kilonzo, nakutuma kwa Bw Musyoka kumwambia asiipotoshe na kuipoteza jamii yetu (Akamba) kisiasa. Hatutafaidika kwa lolote kupitia mwelekeo wa kisiasa anaochukua. Ungana nasi kwenye ‘Hustler Nation’ (Watetezi wa Watu Maskini) kwani ndio utaibuka mshindi kwenye uchaguzi wa 2022,” akasema Bw Muthama.

 

You can share this post!

Mwana anaswa kwa mauaji ya watu 5 wa familia yake

Facebook yaadhibu wafuasi wa Museveni