• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 11:55 AM
Bobi Wine asema majeshi yameteka nyumba yake, serikali yadai inamlinda

Bobi Wine asema majeshi yameteka nyumba yake, serikali yadai inamlinda

CHARLES WASONGA Na MASHIRIKA

MGOMBEAJI urais nchini Uganda Robert Kyangulanyi, maarufu kama Bobi Wine, Ijumaa jioni alidai kuwa wanajeshi wamezingira boma lake eneo la Magere siku moja baada ya uchaguzi mkuu kukamilika.

Kupitia ujumbe katika akaunti yake ya Twitter, mwanasiasa huyo alisema kuwa maafisa hao wanaMtishia maisha kwani hawazungumzi na yeyote.

“Wanajeshi wameruka ua na kudhibiti boma letu. Na hamna anayezungumza nasi. Tuko hatarini. Tuko mateka,” Bw Wine akasema.

Lakini makao makuu ya polisi na yale ya jeshi yalitoa taarifa kukana madai kuwa mgombeaji urais huyo amekamatwa yakisema kuwa kile maafisa wao wanafanya katika boma hilo ni “kumlinda”.

“Ni kweli kwamba maafisa wa polisi na wanajeshi wamezingira makazi yake. Wako nje wala sio ndani lakini…. haja yao kuu ni kuimarisha usalama katika eneo hilo,” Naibu Msemaji wa Polisi katika jiji la Kampala Luke Owoyesigyire akaamba NTV Uganda.

“Hajakamatwa. Tunadumisha usalama katika eneo hilo. Hamna linguine,” akaongeza.

Bw Owoyesigyire aliongeza kusema kuwa watu wawili walijaribu kuruka ua la boma la Bw Wine lakini maafisa waliingilia kati na kukamata mmoja wao ilhali mwingine akatoweka.

Aliongeza kuwa mtu mwingine ambaye alibisha lango la boma hilo, ilhali hakuwa mgeni wao, alikamatwa na kwa ajili ya kuhojiwa ili kubaini nia yake.

“Tukigundua kuwa hawakuwa tisho kwa mheshimiwa na boma lake, wataachiliwa.” Bw Owoyesigyire akaeleza.

Mapema Ijumaa kiongozi huyo wa upinzani alidai uchaguzi huo mkuu ulikumbwa na udanganyifu na fujo nyingi.

Hata hivyo, alielezea imani kwamba atashinda licha ya kwamba kura zilikuwa zikihesabiwa katika mazingira ambapo mawasiliano ya intaneti yalikatizwa kote nchini Uganda.

You can share this post!

Nimeshinda urais kwa kura nyingi mno – Bobi Wine

Uhuru atandika Ruto 3-0