Watu 223 zaidi wapatikana na corona

Na CHARLES WASONGA

WATU 223 Jumamosi walipatika na virusi vya corona ndani ya muda was aa 24 zilizopita baada ya sampuli kutoka watu 7,748 kupimwa.

Kaunti ya Nairobi inaongoza kwa kuandikisha visa vipya 127 ikifuatwa kwa Migori iliyonakili visa 16. Mombasa nayo ina visa 10 vipya huku Kiambu na Meru zikiandikisha visa tisa kila moja, Kajiado (visa 8), Kilifi (6) huku Murang’a na Kericho zikiandikisha visa vine kila moja.

Kulingana na taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Jumamosi alasiri, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alitangaza kuwa wagonjwa wawili zaidi wa Covid-19 walifariki ndani ya saa 24 zilizopita. Idadi hiyo ya vifo sasa imefikisha idadi jumla ya wagonjwa waliangamizwa na Covid-19 nchini kuwa 1,728.

“Hata hivyo, habari njema ni kwamba jumla ya wagonjwa 129 wamepona na kuruhusiwa kurejelea maisha yao ya kawaida; 115 ni wale ambao walikuwa wakiuguzwa nyumbani na 14 ni wale ambao walikuwa wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini,” akasema Bw Kagwe.

Kwa hivyo, idadi jumla ya wale ambao wamepona ni 83,324. Kufikia wakati kama huu wagonjwa 686 wamelazwa katika hospitali mbali mbali huku 1,649 walihudumiwa nyumbani.

Kati ya wagonjwa hao waliolazwa hospitalini, 29 wako katika chumba cha wagonjwa mahututi huku 14 wakipumua kupitia usaidizi wa mitambo maalum kwa jina, “ventilators”.

Habari zinazohusiana na hii