• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 6:55 AM
Uingereza yapendekza wanaougua corona walipwe Sh65,000

Uingereza yapendekza wanaougua corona walipwe Sh65,000

NA AFP

MAAFISA wa Uingereza wanapendekeza kuwa serikali iwalipe watu wanaoambukizwa virusi vya corona ili waweze kukaa nyumbani huku kukiwa na wasiwasi kwamba wengi wanakataa kupimwa na kutozingatia kanuni ya kutotoka nyumbani.

Ingawa mpango huo haujaidhinishwa, inapendekezwa wanaothibitishwa kuambukizwa virusi hivyo walipwe Sh65,000 kwa mwezi. Kwa wakati huu, watu maskini wanalipwa pesa hizo wakiagizwa kujitenga karantini.

Raia wa Uingereza wanapuuza kanuni za kuzuia msambao wa corona zinazotangazwa na serikali ya Waziri Mkuu Boris Johnson.

Mpango huo ambao unaweza kugharimu serikali mabilioni ya pesa kila mwezi unanuiwa kufanya watu kuhofia kupoteza mapato yao wakitakiwa kujitenga wanapothibitishwa kuambukizwa corona.

Waziri wa Mazingira George Eustice alisema hakuna uamuzi ambao umefikiwa kuhusu pendekezo hilo.

Waziri Mkuu Boris Johnson alitarajiwa kuzungumzia suala hilo kwenye kikao na wanahabari Ijumaa.

“Tunataka kuimarisha viwango vya kuzingatia kanuni kwa watu wanaotagamana na walioambukizwa kujitenga, kwa mfano, tunataka watu kupimwa mara moja wakiwa na dalili za virusi hivyo,” Eustice aliambia kituo cha redio cha tl LBC.

“Hii itakuwa gharama kubwa pia,” aliongeza.

You can share this post!

Pigo kwa Jumwa na Tangatanga wakizimwa Kadu

WANDERI KAMAU: Tusimhukumu Trump, tujifunze kutoka kwa...