• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 7:55 AM
Washukiwa saba, silaha 35 zanaswa katika operesheni Kapedo/Arabal

Washukiwa saba, silaha 35 zanaswa katika operesheni Kapedo/Arabal

Na CHARLES WASONGA

WASHUKIWA saba wamekamatwa na maafisa wa usalama wanaoendesha operesheni ya kusaka wahalifu wanaosababisha mauaji katika maeneo ya Kapedo (Turkana) na Arabal (Baringo).

Katika kikao na wanahabari katika makao makuu ya Polisi jumba la Vigilance, Ijumaa, Msemaji wa Polisi Charles Owino alisema kuwa bunduki 35 pia zimenaswa katika operesheni hiyo iliyoanza wiki jana.

“Inasikitisha kuwa tumekuwa tukitoa ulinzi kwa wafugaji hao lakini baadhi yao wamewageukia polisi kwa usaidizi wa watu wenye ushawishi ambao wanafadhili visa vya wizi wa mifugo. Tunawaonya watu kama hawa kwamba siku zao zimehesabiwa kwani tayari tumekamata washukiwa saba na kunasa bunduki 35,” akasema.

Bw Owino alisema kuwa maafisa wa usalama wataendelea na operesheni katika maeneo hayo hadi hali ya utulivu itakaporejea maeneo hayo.

“Kwa hivyo, tunawaomba washukiwa wengine wajisalimishe kwa hiari kabla ya maafisa wetu kukabiliana nao,” akasema.

Kulingana na Bw Owino, wizi wa mifugo umegeuzwa kuwa biashara hatari lakini wahusika wanafuatiliwa “kwa makini na hivi karibuni watakabiliwa na mkono wa sheria.”

You can share this post!

Biden aondoa marufuku ya Trump kuhusu uavyaji mimba

Rais akerwa na utovu wa nidhamu shuleni