Siaya kaunti ya kwanza kupitisha BBI

RUSHDIE OUDIA na CHARLES WASONGA

BUNGE la Kaunti ya Siaya ndilo la kwanza kupitishwa mswada wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano (BBI).

Mswada huo ulipitishwa Jumapili katika kikao maalum cha bunge hilo ambacho pia kilihudhuriwa na Gavana wa Kaunti hiyo Cornel Rasanga Amoth.

Spika wa Bunge hilo George Okode alisema kuwa bunge hilo kupitia Kamati yake ya bunge hilo kuhusu Haki na Masuala ya Sheria iliandaa vikao vya kukusanya maoni ya umma katika maeneo bunge yote sita.

Shughuli hiyo iliendeshwa mchana kutwa mnamo siku ya Jumanne wiki hii.

“Sasa tutawasilisha mswada huu katika Bunge la Kitaifa na Seneti pamoja na ripoti maalum kutoka bunge hili, kulingana na taratibu zilizowekwa,” Bw Okode akawaambia wanahabari baada ya kupitishwa kwa mswada huo.

Kaunti ya Siaya ndiko anakotoka kiongozi wa ODM Raila Odinga ambaye pamoja na Rais Uhuru Kenyatta walifanya handisheki mnamo Machi 9, 2018 iliyopelekea kuungwa jopokazi la BBI.

Mswada huo umepitishwa siku moja baada ya Bw Odinga kukutana na madiwani wote wa chama cha ODM katika eneo la Karen, Nairobi kuwahimiza wapitishe mswada huo.

Kaunti zingi za eneo la Nyanza zimetangaza kuanzisha mchakato wa kuharakisha kupitishwa kwa mswada huo ambao uliwasilishwa na mabunge yote ya kaunti wiki mbili zilizopita.

Mswada huo unahitaji kupitishwa na angalau mabunge 24 kabla ya kushughulikiwa na Bunge la Kitaifa na Seneti kisha uwasilishwe kwa wananchi katika kura ya maamuzi.

Mbunge 47 ya kaunti yanapasa kupitisha mswada huo ndani ya miezi mitatu tangu Januari 26, 2021, IEBC ilipothibitisha kuwa ulipata uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura 1.42 milioni.

Habari zinazohusiana na hii

BBI YAINGIA ICU

Kwani kuliendaje?