• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Klabu 19 kupigania taji la Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda Kaskazini

Klabu 19 kupigania taji la Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda Kaskazini

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

KLAB U 19 za jimbo la Pwani zitashiriki kwenye Ligi ya Taifa Daraja la Pili Kanda ya Kaskazini inyaotarajia kuanza rasmi Jumamosi Februari 6 kwa mechi nne zitakazopepetwa kwenye viwanja mbalimbali.

Katibu wa wa Kanda ya Kaskazini ya ligi hiyo ya FKF, Lilian Nandundu amesema mechi nne zitachezwa Jumamosi na nyingine tano zitafanyika siku ya Jumapili. Lilian amesema mechi zitachezwa viwanja vya Makupa Primary, Samburu, Kombani, Kagombani, Progressive, Alaskan, Shanzu TTC na Bomani MTTI.

Timu hizo 19 zitazoshiriki ligi hiyo ni Ziwani Youth, Sparki Youth, Super Matuga, Samburu Lions, Beach Bay, Yanga, Omax, Wananyuki, Shanzu United, Progressive, Borrusia Dortmund, Bahari, Maji Bombers, Kilifi Allstars, Mariakani FC, Green Marine, Kishada na Nacet FC.

Kutakuwako mechi mbili katika uwanja wa Tudor Primary siku ya Jumamosi ambapo Ziwani Youth ya Mombasa itakutana na Nacet FC kutoka Ukunda kabla ya mechi nyingine kuchezwa uwanjani hapo kati ya Sparki Youth na Kishada FC, zote zikiwa za Mombasa.

Katika uwanja wa Kombani, Kaunti ya Kwale, timu ya hapo nyumbani ya Super Matuga itakabiliana na Green Marine hali timu ya Samburu Lions itawakaribisha majirani zao wa Mariakani FC katika uwanja wa Samburu Kasarani.

Siku ya Jumapili Februari 7, timu za Beach Bay na Kilifi Allstars FC zitakutana kwenye uwanja wa Kagombani Progressive hali katika kiwanja cha Alaskan cha huko Malindi kutakuwa na ‘Malindi Dabi’ kati ya Yanga na Maji Bombers.

Omax, mojawapo ya timu zenye matumaini ya kufanya vizuri katika ligi hiyo, itakutana na Bahari katika uwanja wa Tudor Primary, Wananyuki kuonana na Borrusia Dortmund kutoka Takaungu uwanjani Bomani MTTI hali Shanzu United na Progressive kuchezea uwanja wa Shanzu TTC.

Mwenyekiti wa Omax FC, Farook Khan aliambia Taifale Dijitali kuwa wamepania kuhakikisha wanashinda na kupanda ngazi hadi Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza. “Tunaamini wanasoka wetu wamejiandaa vya kutosha na wametia nia ya kushinda taji la ligi hiyo,” akasema Khan.

Kocha wa Omax FC Ismail Bokassa anasema huwa ni kawaida kwa klabu hiyo ya Omax FC kuwazawadia wachezaji wake kila mwisho wa msimu na hilo linawapa motisha wabnasoka kucheza kwa kujitolea kuihami timu yao.

You can share this post!

Mean Machine na Egerton Wasps waanza kufukuzia tiketi ya...

Ni mashabiki 40 pekee wataruhusiwa kushuhudia mechi