• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Biden aahidi kushirikiana na Afrika

Biden aahidi kushirikiana na Afrika

Na AFP

WASHINGTON, Amerika

RAIS wa Amerika Joe Biden Ijumaa aliahidi kushirikiana na Afrika katika nyanja mbalimbali huku akiahidi kuhudhuria Mkutano wa ana kwa ana wa viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) siku zijazo.

Katika ujumbe kupitia njia ya video kwa mkutano wa AU unaendeshwa kwa njia ya mtandao kutokana na janga la corona, Rais huyo kwa mfano aliahidi kushirikiana na Afrika katika nyanja za kupambana na homa hiyo na mabadiliko ya hali ya anga kando na kupiga jeki juhudi za kukomesha mapigano katika mataifa mbalimbali ya bara hili.

“Japo hii haitakuwa rahisi, Amerika iko tayari kuwa mshirika wenu, msaidizi na rafiki wa kweli,” Biden akasema. “Ni matumaini yangu kuwa nitakuwa nanyi ana kwa ana wakati mwingine,” akaongeza.

Hii ni kinyume na mtangulizi wake Donald Trump ambaye alionekana kutojihusisha na masuala ya Afrika katika kipindi chake cha miaka minne uongozini.

Biden ameahidi ambaye aliapishwa mnamo Januari 20, 2021 ameapa kuendeleza demokrasia na haki za walio wachache—ambao mara nyingi hubaguliwa na kudhulumiwa barani Afrika.

Bidena alisema kuwa anataka kufanyakazi na Afrika “katika kuwekeza katika uimarishaji wa taasisi zetu za kidemokrasia na kuendeleza haki za kibinadamu kwa watu wote— wanawake na wasichana, wanapenzi wa jinsia moja, walemavu na watu wa asili ya makabila, dini na matabaka yote.”

Rais Trump ndiye rais wa kwanza wa Amerika baada ya rais wa zamani Ronald Reagan, ambaye hajawahi kuzuru Afrika katika utawala wake.

Trump alinukuliwa mara kadha akitumia lugha chafu kurejelea mataifa ya Afrika alipokuwa akielezea mantiki ya sera yake ya kuzuia hawahamiaji wasio weupe kuingia Amerika.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Rais wa Masumbwi yasiyo ya malipo duniani kuwasili Kenya...

Agizo wahudumu wa afya waondoke nyumba za serikali