• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Meneja aliyeghushi vyeti atafune mamilioni abubujikwa na machozi kortini

Meneja aliyeghushi vyeti atafune mamilioni abubujikwa na machozi kortini

Na Richard Munguti

MENEJA mkuu katika Mamlaka ya Kitaifa ya Usambazaji Stima Mashambani (REA), Ijumaa alisababisha kioja mahakama ya Milimani Nairobi alipolia ikawa vigumu kusomewa mashtaka 13 ya kughushi vyeti vya digrii na sekondari.

Mbali na mashtaka hayo ya kughushi vyeti vya chuo kikuu na sekondari, Bi Irene Chesang alikabiliwa na mashtaka mawili ya kupokea kwa njia ya undanganyifu mishahara ya zaidi ya Sh10.9 milioni kutoka kwa REA na shirika la ustawishaji wanyama wapori (KWS).

Ilimlazimu hakimu mkuu mahakama ya kuamua kesi za ufisadi Douglas Ogoti kuamuru Bi Irene Chesang arudi nyumbani kujipa moyo na kujihoji kabla ya kujibu mashtaka ya ufisadi.

Wakili Evans Ondieki anayemwakilisha Bi Chesang aliomba mahakama impe muda mshtakiwa ajihoji kisha atulie kabla ya kusomewa mashtaka.

Mshtakiwa anadaiwa alighushi cheti cha digirii aliyodai alihitimu mnamo Juni 17 2000.

Mshtakiwa alishtakiwa alimkabidhi Bi Rose Mkalama cheti hicho cha digirii akijua hajahitimu kufanya kazi katika mamlaka hiyo ya REA.

 

You can share this post!

BBI yapanua ufa Bonde la Ufa

DOUGLAS MUTUA: Polisi pia ni watu, watunzwe ndipo wapate...