• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Mihadarati yawanyima vijana nafasi jeshini

Mihadarati yawanyima vijana nafasi jeshini

Na SIAGO CECE

IDADI kubwa ya vijana katika Kaunti ya Mombasa wamekosa nafasi kujiunga na jeshi la taifa (KDF) kwa sababu ya utumizi wa mihadarati.

Kulingana na Afisa Mkuu wa Usajili wa makurutu wa jeshi Luteni Kanali Benjamin Kiprop, wengi walifeli katika hatua ya ukaguzi wa kiafya baada ya kubainika kuwa hawafai.

Hali hiyo imeshuhudiwa tangu shughuli hiyo ilipoanza mapema wiki hii.

“Kwa siku tatu zilizopita, shida moja kuu ni kwamba, baadhi ya vijana walibainika kuwa waraibu wa mihadarati. Hii ndio maana matokeo ya uchunguzi wa kiafya yalibaini kuwa hawafai kuhudumu jeshini,” afisa huyo akasema.

Kando na uchunguzi wa kiafya, vijana waliojitokeza pia walipimwa uzani, kimo na ubora wa viungo vya mwili kabla ya kukimbia kwa umbali wa kilomita tano.

Shughuli hiyo iliyoanza Jumatano kote nchini inalenga kuwasijili Wakenya 4,400 kujiunga na KDF.

Katika kaunti ya Mombasa, shughuli ya usajili wa makurutu jana iliendelea katika eneo la Mikindani na leo itafanyika katika eneo bunge la Nyali.

Mwaka huu KDF itasajili maafisa wa vitengo sita. Licha ya kuwepo kwa idadi kubwa ya vijana wenye shahada za digrii lakini hawana ajira nchini, Mombasa haikuweza kutoa watu waliohitimu kuajiriwa kama maafisa wa makadeti, ambapo ni watu wawili pekee walijitokeza.

Hakuna kijana yeyote mwenye digrii aliyejitokeza katika kaunti ndogo ya Changamwe.

You can share this post!

Wanafunzi kufanya mitihani chini ya CBC

BI TAIFA FEBRUARI 11, 2021