• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:20 AM
Shujaa na Lionesses kuelekea Uhispania usiku wa kuamkia Jumapili kwa raga ya kimataifa

Shujaa na Lionesses kuelekea Uhispania usiku wa kuamkia Jumapili kwa raga ya kimataifa

Na GEOFFREY ANENE

TIMU za taifa za raga za wachezaji saba kila upande za Kenya Shujaa (wanaume) na Lionesses (wanawake) Jumamosi usiku zinaelekea nchini Uhispania kwa mashindano ya kimataifa.

Shujaa ya kocha Innocent ‘Namcos’ Simiyu italimana na Amerika ya kocha Mike Friday, Ufaransa, Argentina, Ureno na wenyeji Uhispania katika raundi ya kwanza mnamo Februari 20-21 jijini Madrid.

Timu hizo zote isipokuwa Ureno zinashiriki Raga za Dunia. Kenya, Amerika na Argentina pia zimefuzu kushiriki michezo ya Olimpiki jijini Tokyo, Japan mwezi Julai/Agosti mwaka huu.

Lionesses, ambayo inanolewa na Felix Oloo, itapepetana na Amerika, Ufaransa, Urusi, Uhispania na Poland siku hiyo. Mashindano yote mawili yatachezwa kwa njia ya mzunguko.

VIKOSI: Lionesses – Philadelphia Olando (nahodha), Celestine Masinde, Sheila Chajira, Ann Goretti, Stella Wafula, Naomi Amuguni, Camilla Cynthia, Janet Okello, Linet Moraa, Enid Ouma, Diana Awino, Christabel Lindo, Sarah Oluche; Shujaa – Nelson Oyoo (nahodha), Herman Humwa (nahodha), Alvin Otieno, Bush Mwale, Harold Anduvati, Vincent Onyala, Willy Ambaka, Daniel Taabi, Johnstone Olindi, Mark Kwemoi, Tony Omondi, Billy Odhiambo, Derrick Keyoga, Jacob Ojee, Jeff Oluoch Non Travelling reserve: Alvin Marube.

RATIBA:

Lionesses

20 Februari

12.22pm Russia na Lionesses

2.45pm Amerika na Lionesses

5.30pm Ufaransa na Lionesses

21 Februari

12.22pm Spain na Lionesses

3.29pm Poland na Lionesses

Shujaa

20 Februari

1.50pm Shujaa na Ufaransa

4.35pm Shujaa na Ureno

7.20pm Shujaa na Amerika

21 Februari

1.28pm Shujaa na Uhispania

4.13pm Shujaa na Argentina

You can share this post!

RB Leipzig wamsajili beki Angelino kutoka Manchester City

AKILIMALI: Mfumo wa Hydroponic na mbinu asilia kukabili...