• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 5:23 PM
Makazi ya kocha Ancelotti yavamiwa mjini Merseyside, Uingereza

Makazi ya kocha Ancelotti yavamiwa mjini Merseyside, Uingereza

Na MASHIRIKA

MAKAZI ya kocha Carlo Ancelotti wa Everton yalivamiwa na majambazi usiku wa kuamkia Jumamosi na kijisanduku kilichokuwa na pesa kiasi kisichojulikana kuibwa katika eneo la Hall Road East, Crosby, Merseyside, Uingereza.

Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, hakuna mtu yeyote katika makazi hayo aliyejeruhiwa.

Maafisa hao wa polisi sasa wanafanya uchunguzi na wameomba yeyote aliye na habari kuhusu majambazi hao waliokuwa wamevalia mavazi yaliyowafunika hadi usoni kuwapa vidokezi.

Ancelotti ambaye ni raia wa Italia aliteuliwa kuwa kocha wa Everton mnamo Disemba 2019 na akatia saini mkataba wa miaka minne na nusu uwanjani Goodison Park. Kandarasi hiyo ya Ancelotti inatarajiwa kutamatika mwishoni mwa msimu wa 2023-24.

Ancelotti, 61, anajivunia kunyanyua jumla ya mataji 20 katika historia yake ya ukufunzi.

Miongoni mwa mataji hayo ni manne ya Ligi Kuu katika mataifa manne tofauti na mawili ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) akidhibiti mikoba ya AC Milan ya Italia na Real Madrid, Uhispania.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

MAPISHI: Maharagwe yenye tui la nazi

Leicester City watoka nyuma na kuendeleza masaibu ya...