• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Askofu asema corona imewapa Wakenya fursa ya kumtambua Mola

Askofu asema corona imewapa Wakenya fursa ya kumtambua Mola

Na Stephen Munyiri

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Dayosisi ya Nyeri Anthony Muheria amesema kuwa ujio wa virusi vya corona umewafungua macho Wakenya ili wazidishe ibada na kutegemea zaidi Mwenyezi Mungu.

Mtumishi huyo ambaye pia alilazwa hospitali ya Mater, Novemba mwaka jana baada ya kuambukizwa corona, alisema kuwa uwepo wa ugonjwa huo umedhihirishia binadamu uwezo mkuu wa Mungu.

Alisema binadamu sasa wameona nuru na kuamini kuwa uwezo wa Mungu ni mkuu mno na ndiye anawaondolea binadamu mikasa.

Askofu huyo alikuwa akihutubu wakati wa warsha iliyoandaliwa na vyuo vikuu vya Aga Khan na Karatina wikendi. Warsha hiyo ilifanyika ili kuwahamasisha watu dhidi ya virusi vya corona.

Kulingana naye, hapo awali watu walikuwa hawatambui utukufu wa Mungu lakini ujio wa corona umetoa nafasi kwa binadamu kuokolewa na kuzidisha imani ili kushinda janga hilo.

“Mara ya kwanza niliposikia kuhusu corona ni Disemba 2019 na nilifikiria kuwa ulikuwa ugonjwa wa China pekee. Nilifikiria kuwa nisingefikiwa lakini miezi michache baadaye nilifikiwa nao. Corona ipo na kila mmoja anafaa ajihadhari,” akasisitiza Askofu Muheria.

 

You can share this post!

West Brom wakaba koo Man-United na kudidimiza matumaini yao...

Bei ya mafuta kupandisha gharama ya maisha