• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 4:55 PM
Madiwani wa Nyeri watiwa presha wapitishe BBI

Madiwani wa Nyeri watiwa presha wapitishe BBI

NA MWANDISHI WETU

MADIWANI wa Kaunti ya Nyeri wametakiwa kuidhinisha mswada wa BBI la sivyo wote watang’olewa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2022.

Wakati wa hafla za kutoa maoni kuhusu BBI zilizofanyika katika kaunti ndogo nane kwenye kaunti hiyo, wakazi walijitokeza kwa wingi kutoa maoni yao. Wakazi hao waliunga mkono marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI.

Mwakilishi wa mchakato huo wa BBI aliye pia mbunge wa zamani wa Mathira Bw Peter Weru aliyehudhuria hafla hiyo ya utoaji maoni mjini Karatina alisema wananchi walikuwa wamepotoshwa kuhusu mchakato huo na kwamba wamebadilisha maoni baada ya kuelezwa ukweli kuhusu malengo ya BBI.

Bw Weru alisema kulingana na idadi kubwa ya watu waliojitokeza ni dhahiri mabadiliko yaliyopendekezwa yameidhinishwa.

Katika eneo la Nyeri ya kati, wananchi wakiongozwa na Mbunge wa eneo hilo Bw Ngunjiri Wambugu walisema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawafaidi wananchi na eneo hilo.

Bw Thuo Mathenge atakayewania Ugavana Nyeri alisema yeyote anayepinga BBI ni adui mkuu wa mchakato huo na pia maendeleo.

Alisisitiza kuwa lazima kaunti ya Nyeri iidhinishe mswada huo la sivyo MCAs wanakabiliwa na tisho la kubanduliwa.

Eneo la Kieni, mbunge wa eneo hilo Kanini Kega na kundi la MCAs waliongoza wakazi wa eneo hilo kutoa maoni yao katika ukumbi wa kanisa la Katoliki Narumoru.

You can share this post!

Kaunti ya Nairobi pia yapitisha BBI

Achuma hela kwa kutia nakshi vinyago Mombasa