• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 2:55 PM
Serikali yaonya mvua yaja mwezi ujao kwa kishindo kikuu

Serikali yaonya mvua yaja mwezi ujao kwa kishindo kikuu

NA COLLINS OMULO

TAHADHARI imetolewa kuwa msimu wa mvua utakaoanza Machi utakuwa na kiwango kikubwa cha mvua kuliko kawaida.

Idara ya serikali inayosimamia masuala ya utabiri wa hali ya hewa na tabia nchi katika eneo la IGAD (ICPAC), imesema mvua hiyo itanyesha hasa Magharibi mwa nchi kuanzia Machi hadi Mei.

Mvua hiyo inatarajiwa kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutakuwa na baridi nyingi Magharibi ya nchi wakati wa mvua hiyo itakayoshuhudiwa kwa miezi mitatu.

Wakati huo huo, maeneo ya Mashariki ya Kenya yatapokea mvua kidogo na kiangazi kisicho cha kawaida.Mito Ewaso Ngiro, Tana na Athi inatarajiwa kufurika na kuvunja kingo zake huku pia hali kama hiyo ikishuhudiwa katika katika Ziwa Kerio na lile la Turkwel.

Wakazi wanaoishi karibu na Ziwa Viktoria pia wametahadharishwa kuwa kiwango cha maji katika ziwa hilo kitapanda na kusababisha mafuriko na kuharibu miundomsingi.Mvua kadri imekuwa ikishuhudiwa maeneo ya Ziwa Viktoria na Bonde la Ufa.

Kaunti za Busia, Siaya, Kisumu, Kericho, Homa Bay, Bomet, Kisii, Migori, Nyamira, Narok, Nairobi na Kajiado.

 

You can share this post!

Raila ataka kesi za kupinga BBI zitupiliwe mbali

BENSON MATHEKA: Wabunge wasitunge sheria kulenga mirengo ya...