• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 7:50 AM
FATAKI: Imarisha chombo chako uweze kupiga mbizi baharini badala ya kulalama bure!

FATAKI: Imarisha chombo chako uweze kupiga mbizi baharini badala ya kulalama bure!

NA MWANDISHI WETU

Kuna tabia ambayo imekithiri miongoni mwa madume. Nazungumzia ile tabia ya kutumia neno kisima kumaanisha uke wa mwanamke uliopanuka. Hasa maana hii hujitokeza zaidi wanapotumia neno la Kiingereza “borehole”.

Ni hali niliyoshuhudia majuzi kwenye Facebook madume fulani walipotofautiana na binti mmoja kimawazo na wakaamua kutupia neno hilo kumzima.

Lakini mjadala wetu hii leo sio kuhusu kisa hicho, bali kukemea tabia hii mbovu ya baadhi ya wanaume ya kumzima mwanamke kwa kutaja upana au ukubwa wa uke wake iwe amewahi kuwaburudisha au la.

Katika enzi za sasa inashangaza kwamba bado kuna madume wanaodhani kwamba thamani ya mwanamke inapimwa kwa wembamba au upana wa uke wake.

Hawa ni madume wanaodhani kwamba udogo wa sehemu hii ndio huongeza ladha ya mahaba.Hawa ni akina kaka wachanga katika masuala ya kimahaba, waliozoea kuogelea kwenye vidimbwi vidogo vinavyojikusanya mitaani baada ya mvua kunyesha.

Hivyo kutokana na ujuzi wao finyu usiowawezesha kuogelea kwenye bahari au ziwani, basi wanaunda uadui.

Hawa ni madume wanaosahau kwamba mahaba huhusisha pande zote mbili; yaani, uwezo wa kufikia maji kisimani na kuyafurahia, utategemea sio tu hali ya kisima, bali pia urefu wa kamba unayotumia kuteremshia chombo cha kutekea maji.

Kama nilivyosema wakati mmoja, wanaosisitizia sana uthabiti wa sehemu hii, husahau kwamba wembamba na udhaifu wa uzi, kamwe haupaswi kutumika kama kisingizio cha kuelekezea lawama tundu la sindano.Ikiwa haufikii kina cha kisima, basi huenda hauna ujuzi wa kufanya hivyo, au chombo chako ni kidogo.

Kwa hivyo badala ya kuzama kwenye ziwa au bahari, pengine unapaswa kurejea kuogelea kwenye vidimbwi vidogo vya mvua huko mtaani.

Badala ya kulalama kwamba kisima ni kipana au kina chake ni kirefu, wajichunguze iwapo kwa kweli wana uzi au ni kamba yenye nguvu ya kutosha kukuteremshia chombo chako kisimani, na kutekea maji ya kutosha.

Hata wachimba visima watakuambia kwamba kuna aina mbalimbali za visima kuambatana na upana na kina. Kwa hivyo kama mteka maji, unapaswa kuendea kisima kinachoambatana na urefu na uthabiti wa kamba yako. Kumbuka kwamba ajuaye kuogelea hawezi lalamika kuhusu upana au kina cha mto.Bila shaka haimaanishi kwamba sehemu hii isishughulikiwe.

La! Lazima vichaka vinavyozingira sehemu hii viondolewe, kuta zishughulikiwe na kuwa thabiti ili usafi wa maji udumishwe. Lakini kama mwanaume, hauna haki ya kumtusi wala kumkejeli mwanamke kwa misingi ya hali ya uke wake!

You can share this post!

MWANAUME KAMILI: Haiwezekani kushiriki uovu ukaepuka dosari!

FUNGUKA: Msisimko wangu wa mahaba hutokana na kutazama...