• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:47 AM
KENNEDY WAMBUA: Tambua mtindo mpya wa usanii ‘Kambacha’

KENNEDY WAMBUA: Tambua mtindo mpya wa usanii ‘Kambacha’

Na JOHN KIMWERE

MWANZO wa ngoma kila mja hujipa matumaini ambapo huwa ni hali ya kutarajia. Ni katika kutumainia na kuvumilia ambapo ana imani nyota yake itang’aa na kutinga upeo wa mwana muziki wa kimataifa miaka ijayo.

Kennedy Wambua Muvea ambaye kwa jina la msimbo anafahamika kama Kennybizzoh ni miongoni mwa wasanii wanaoendelea kuvumisha jukwaa la muziki wa injili nchini.

Ni kati ya waimbaji muziki kwa mtindo wanaoita ‘Kambacha’ unaokwenda sawia na mitindo ya wana muziki kutoka mataifa mengi kama Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Rwanda kati ya mengine.

Nyimbo ya kwanza kwa mtindo huo kwa jina ‘Ngai Wakwa,’ aliomshirikisha mwanamuziki Stephen Kasolo aliitunga mwaka 2017. Stephen Kasolo alipata umaarufu kutokana kibao chake kilichokwenda kwa jina ‘Kitole.’

Kennybizzoh alianza kujituma katika masuala ya muziki mwaka 2015 alipotunga na kurekodi kibao cha kwanza kwa jina ‘Mungu ni Mungu’ akitumia mtindo wa Afro-Vision na Bongo katika utunzi wake.

”Katika mpango mzima ninashukuru Mungu kwa umbali ambao nimetoka hazijakuwa shughuli rahisi. Kiukweli ameniwezesha kupiga hatua katika masuala ya muziki ambapo ninaamini ningali ninayo nafasi ya kufanya vizuri zaidi,” alisema na kuongeza kuwa kwa sasa anazidi kuvumisha mtindo wa kambacha.

Mapema mwezi huu msanii huyu aliachia teke inayokwenda kwa jina ‘Masati,’ inayoendelea kupokelewa vizuri na wapenzi wa nyimbo za kumtukuza Mungu.

Chipukizi huyu ambaye anajivunia kutunga na kurekodi nyimbo kama; ‘Hawezi Shindwa,’ ‘Mwaki (Moto),’ ‘Kimena (Chuki)’, ‘Loving You’, ‘Walala(Wonderfull)’, ‘Mzazi’ na ‘Ngai wakwa(Mungu wangu)’ kati ya zingine.

”Hatua yangu kutunga nyimbo za Kikamba ninahisi nimetimiza mojawapo kati ya maazimio yangu. Katika mpango mzima kwa nguvu zake Maulana ninapania kuendelea kuachia nyimbo zaidi kwa lugha ya mama,” akasema.

Msanii huyu anasema kuwa mwaka huu wafuasi wake watarajie nyimbo moja baada ya nyingine. Anadokeza kuwa anatarajia kufanya kolabo nyingi tu ndani na nje ya nchi pia miradi zingine.

Anadokeza kuwa analenga kutinga upeo wa kimataifa kwa kueneza utamaduni wa Kenya kupitia nyimbo za mchanganyiko wa lugha mbali mbali ikiwamo Kikamba na Kiswahili.

Kadhalika anashikilia kuwa anauwezo tosha kufanya muziki na ukumbalike ndani ya muda mchache. Kenny Bizzoh anasema anapenda kujifunza mengi kutokana na kazi za wenzake.

Anadokeza anapenda kuketi kusikiliza nyimbo kama ‘Vanity’, ‘Defender’, na ‘Nisamehe’, ‘Mitego,’ tugho za waimbaji Daddy Owen na Kaberere mtawalia. Msanii huyu alifunga pingu za maisha mwaka 2019 ambapo tayari wamebarikiwa na mtoto mmoja.

  • Tags

You can share this post!

Fujo tena katika mikutano ya Ruto na Raila

HARRIET KWAMBOKA: Ipo siku nitatesa katika tasnia ya...