UDAKU: Mke wa zamani wa Mahrez ameamua kuuza picha za uchi

Na CHRIS ADUNGO

KIPUSA Rita Johal ambaye alikuwa mke wa mwanasoka wa Manchester City na timu ya taifa ya Algeria, Riyad Mahrez, sasa anauza video na picha za uchi wake mtandaoni.

Demu huyo alianzisha ‘biashara’ hiyo wiki jana, siku chache baada ya kutoka korokoroni alimokuwa kwa kukiuka kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona jijini London, Uingereza.

Rita, 28, alikuwa katika kundi la vipusa waliohudhuria hafla ya kuponda raha usiku kucha jijini London kinyume na sheria. Alitozwa faini ya Sh4.2 milioni, pesa ambazo alisema zilipunguzwa na maafisa wa usalama kutokana na “urembo wangu wa kupindukia”.

Akitumia akaunti yake ya Instagram wiki jana, Rita aliwataka zaidi ya mashabiki wake 500,000 wa kiume kupata “uhondo” kwa kutazama picha na video zake kwa ada ya Sh1,200 kila mwezi.

Ina maana kwamba iwapo nusu ya majanadume hayo yote yatatazama “zawadi” hizo za mitandaoni, basi mwanamitindo huyo raia wa Uingereza atakuwa akitia mfukoni Sh300 milioni kila wiki nne.

Kufikia Ijumaa wiki iliyopita, Rita alikuwa amepakia mtandaoni video 16 na picha 12.

“Uhondo” huo ulichangamsha malaki ya mashabiki wake waliomhimiza “asichoke kuwaburudisha”.

Mahrez, 29, alimtema Rita mnamo Agosti mwaka jana baada ya kudumu katika ndoa kwa kipindi cha miaka sita, na kumvisha mwanafasheni na mwigizaji Taylor Ward pete ya uchumba jijini Paris, Ufaransa.

Sogora huyo wa zamani wa Leicester City alichukua hatua hiyo baada ya kudumu na Rita katika ndoa kwa kipindi cha miaka sita.

Kiini cha Mahrez kumtema Rita ni jicho la nje la kichuna huyo aliyewahi kukiri kuandamwa na kunyemelewa mitandaoni na wanamichezo wa haiba kubwa waliopagawishwa na urembo wake.

Rita aliwahi kumwonjesha asali bondia raia wa Uingereza, Anthony Joshua, kabla ya tunda lake kudokolewa pia na mwanandondi wa Amerika, Deontay Wilder mwaka jana. Demu huyo mwenye asili ya India, alifunga pingu za maisha na Mahrez katika ndoa ya siri iliyoandaliwa Agosti 2015 na wamejaliwa watoto wawili. Mwanambee wao ni binti anayeitwa Inaya.

Michepuko ya Rita ilimchochea Mahrez kuanza kumtambalia Taylor kimapenzi na aliwahi kumpangia sherehe iliyogharimu Sh700,000 na marafiki 15 wa kichuna huyo katika mkahawa wa Ivy Asia jijini Manchester, Uingereza mnamo Oktoba 2020. Tangu wakati huo, Mahrez na kidege chake wamekuwa wakila bata mara kwa mara katika hoteli ya China White, Uingereza.

Buyu la asali la Taylor, 23, limewahi pia kutikiswa na Sergio Aguero wa Man-City, Mason Holgate wa Everton na mwigizaji Sam Reece, 27. Ashley Ward, 50, ambaye ni babaye Taylor, ni sogora wa zamani wa Crewe Alexandra, Barnsley, Man-City na Leicester ambayo Mahrez alichezea kabla ya kutua ugani Etihad.

Mwishoni mwa mwaka uliopita, Taylor alipakia mtandaoni picha alizopigwa kwa pamoja na Mahrez wakiponda raha katika Kisiwa cha Sardinia, Italia na kusisitiza kwamba kubwa zaidi katika matamanio yake kwa sasa ni kufunga pingu za maisha na sogora huyo ndipo aanze kumfyatulia vimalaika.