• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Chifu awanyima wanasiasa wawili fursa ya kutumia maikrofoni kuhutubu mazishini

Chifu awanyima wanasiasa wawili fursa ya kutumia maikrofoni kuhutubu mazishini

Na SAMMY KIMATU

WAOMBOLEZAJI katika hafla ya mazishi walishuhudia kisa ambapo chifu aliwanyima wanasiasa wawili fursa ya kuhutubu kwa kutumia maikrofoni.

Badala yake, chifu wa eneo hilo aliwaalika kwenye jukwaa na kuwaambia wasalimie waliohudhuria mazishi hayo kwa kuwapungia waombolezaji.

Baada ya kuwaita mbele katika jukwaa, aliomba wawili hao wasalimiane pamoja kisha wapigwe picha ya pamoja.

Tukio hilo lilitokea wakati wa hafla ya mazishi ya mkulima maarufu marehemu Bw Samuel Nzioka Mallei katika Ukumbi wa Nduu ulioko kwenye maeneo ya tarafa ya Mutituni.

“Wanafamilia na kanisa hawakuwa na nafasi ya siasa katika programu yao. Ninawauliza mje hapa jukwaani mwapungie watu mikoni bila kuongea kisha mpigwe picha ya pamoja mkisalimiana, ’’ Bw Musyoki Mallei, naibu mkuu wa chifu katika eneo la Nduu alisema.

Mwanafamilia, Bw Judmaier Mwanzia Nzioka alisema familia ilifikia uamuzi huo kwani walitaka kumpumzisha baba yao mpendwa kwa amani na hawangeweza kutaka siasa ziletwe mazishini.

Kulingana na kanisa lililoongoza na liliendesha ibada hiyo, African Brotherhood Church Mutituni, ni kinyume cha sheria kuleta siasa kwenye mazishi ambapo familia zinaomboleza watu wao wa familia waliofariki.

You can share this post!

Simba aua mbuzi na kondoo katika vijiji kadhaa Lamu

Leicester City wana kila sababu ya kumaliza kampeni za EPL...