• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:38 AM
Nafasi ipo kuimarisha BBI iwafae Wakenya – Mudavadi

Nafasi ipo kuimarisha BBI iwafae Wakenya – Mudavadi

Na SAMMY WAWERU

KINGOZI wa ANC Bw Musalia Mudavadi amesema Ripoti ya Mpango wa Maridhiano (BBI) ingali na nafasi kuimarishwa licha ya serikali za ugatuzi kuidhinisha ielekee bunge la kitaifa na seneti kujadiliwa ili kura ya maamuzi kuandaliwa.

Kufikia Jumanne, kaunti 38 zilikuwa zimepiga kura kuidhinisha Mswada huo wa Marekebisho ya Katiba 2020.

Bw Mudavadi amesema kabla kura ya maamuzi kuandaliwa, kuna nafasi BBI kujadiliwa ili mapendekezo yaliyo kwenye mswada huo yasaidie kuimarisha maisha ya Wakenya.

Huku BBI ikielekea bungeni, kiongozi huyo wa ANC alisema viongozi na wanasiasa wanaoipinga wana muda kutoa mapendekezo.

“Bado kuna nafasi ya Wakenya waafikiane tuiimarishe,” akasema Bw Mudavadi.

Alisema hayo Jumanne usiku, kwenye mahojiano na runinga ya Citizen.

Akionekana kulenga wanasiasa ambao wamekuwa wakikosoa ripoti hiyo ya maridhiano, Bw Mudavadi alisema baadhi yao wamekuwa wakiingiza siasa ili kuisambaratisha.

“Serikali za kaunti zimeidhinisha BBI, walioingiza siasa mchezo huo sasa umeisha, i mikononi mwa Wakenya na ndio wataamua,” akasema.

Licha ya serikali za ugatuzi kupitisha mswada huo, kuna kesi saba zilizowasilishwa mahakamani kuupinga.

BBI ilibuniwa baada ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga kutangaza kuzika tofauti zao za kisiasa mnamo Machi 2020, kupitia salamu za maridhiano maarufu kama Handisheki.

You can share this post!

Bayern Munich waponda Lazio 4-1 kwenye mkondo wa kwanza wa...

Giroud asaidia Chelsea kuzamisha Atletico Madrid kwenye...