• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 11:55 AM
Taabani kwa kuuza vifaa feki vya kupima Ukimwi

Taabani kwa kuuza vifaa feki vya kupima Ukimwi

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYABIASHARA watatu Jumatatu walifikishwa kortini wakikabiliwa na mashtaka kuuza vifaa feki vya kupima Ukimwi.

Mabw Erick Ndung’u Mwangi , Jones Oluoch na Robert Njoya walishtakiwa mbele ya hakimu mkuu mahakama ya Milimani Bi Martha Mutuku.

Kwa nyuso zilizokuwa zimelowa aibu watatu hao wakiinamisha vichwa vyao walikanusha mashtaka kadhaa dhidi yao.

Kwa shtaka la kwanza wote wataty Mabw Mwangi, OIuocha na Njoya walikana walikuwa wakiwauzia watu vifaa bandia vya kupima ugonjwa hatari wa Ukimwi.

Kiongozi wa mashtataka Bw Anderson Gikunda alieleza mahakama kuwa watatu hao walikuwa wanawauzia wananchi vifaa hivi kujipima ukiwmi.

Walishtakiwa kupatikana wakiwauzia wananchi jijini Nairobu vifaa bandia vya kupima Ukimwi kinyume cha sheria cha kuuza bidhaa duni. Shtaka la pili lilikuwa dhidi ya Erick Ndung’u Mwangi.

Hakimu mkuu (kushoto) na kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda. Picha/RICHARD MUNGUTI

Alishtakiwa mnamo Desemba 30 2019 katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta aliuzia nchi ya Guyana Amerika kusini patiki 400 za vifaa hivyo feki vyenya thamani ya Sh800,000.

Shtaka la tatu dhidi ya Erick lilisema katika uwanja huo wa ndege wa JKIA alikamatwa akiwa na shehena nyingine ya vifaa hivyo bandia vya kupima ukimwi kinyume cha sheria.

Njoya ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Intercare Agencies iliyoko barabara ya Duruma Nairobi alipatikana amehifadhi pakiti za vifaa feki za kupima ukimwi zenye thamani ya Sh12,5000.

Walikanusha mashtaka na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000.

Bi Mutuku aliamuru kesi hiyo itajwe baada ya wiki mbili Bw Gikunda aeleze ikiwa amewakabidhi washtakiwa nakala za kesi hiyo pamoja na cheti cha mashtaka.

You can share this post!

Sonko adai kuna mtu alitaka kumdunga sindano ya sumu

Majaji 5 wazima mpango wa BBI