• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Maafisa wa kaunti motoni kwa kupatikana na silaha

Maafisa wa kaunti motoni kwa kupatikana na silaha

Na RICHARD MUNGUTI

WAFANYAKAZI wawili wa Kaunti ya Marsabit pamoja na raia wawili wa Ethiopia walishtakiwa jana kwa kupatikana na silaha hatari.

Mabw Mohamed Galmagar na Ibrahim Abduba Galma ambao ni wafanyakazi wa kaunti hiyo walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi Bw Bernard Ochoi pamoja na Mabw Galma Jara na Musa Dalacha ambao ni raia wa Euthiopia.

Mwakilishi wa wadi ambaye alitarajiwa kushtakiwa pamoja na wawili hao hakufika kortini na mahakama ilitoa kibali atiwe nguvuni.

Bw Galmagar ameajiriwa na kaunti ya Marsabit kama dereva ilhali Galma ni Mekanika katika gatuzi hilo.

Wote wanne walikabiliwa na shtaka la kupatikana na bunduki na raundi 10 za risasi bila idhini kutoka kwa asasi inayohusika na umiliki wa silaha.

Kiongozi wa mashtaka Bw Anderson Gikunda alieleza mahakama wanne hao walitiwa nguvuni katika eneo la Ele Borr kaunti ndogo ya Turbi wakiwa na silaha hizo mnamo Feburuari 6 2021.

Raia hao wa Ethiopia walishtakiwa kwa kosa la kupatikana wakiwa nchini bila idhini kutoka kwa idara ya uhamiaji.

Abduba na Galma waliachiliwa kwa dhamana ya Sh300,000 pesa tasilimu kila mmoja na raia hao wa kigeni wakazuiliwa katika gereza la viwandani kwa vile mahakama ilielezwa hawana mahala rasmi pa kuishi nchini.

You can share this post!

SGR ya Kisumu kukamilika 2022

Kipchoge kurejea Ujerumani kujiandaa kwa Hamburg Marathon