• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
DOMO KAYA: Leo hii kajifanya mbogo!

DOMO KAYA: Leo hii kajifanya mbogo!

Na MWANAMIPASHO

HIVI umewahi kusikia ule msemo kuwa adui ya mwanamke ni mwanamke?

Huyu aliyeibuka na semi hii lazima alikuwa ameyaona matukio mengi ya wanawake kuoneana wivu. Ndiko aliko kwa sasa soshiolaiti Huddah Monroe. Juzi kati kaanzisha bifu na Tanasha Donna, kisa mwenzake kusherehekea kutimiza ‘Followers’ milioni tatu kwenye Instagram.

Baada ya Tanasha kuposti akiwashukuru mashabiki wake hao, mwenzake huyo alitupia ndongo akijifanya kushangaa ikiwa bado watu husherehekea wanapopata ‘followers’ wengi. Kwa maneno yake, Huddah mwenye followers 2.1 milioni alijigamba ni bora kuringa kwa kuwa na hela kuliko kujigamba kwa kupata followers.

Sielewi kabisa machungu ya yake kwa Tanasha yanatokea wapi. Mwanzo kabisa kuna tatizo gani Tanasha kufurahia kupata ‘followers’ milioni 3? Lakini pili watu kama Huddah ambao hujigamba kuwa wana hela ndio wale huwa hawana kakitu. Si wajua tena, debe tupu ndio huwa na kelele la kishindo.

Kumwona akimchamba mwenzake bila sababu inanisikitisha. Hivi Huddah zaidi ya urembo wake anaweza kututajia mafanikio gani aliyoyapata? Kheri Tanasha anayejitahidi kuimba angalau apate riziki na pia akifanya kazi za matangazo biashara. Unawezaje kumlinganisha mtu wa aina hii na sampuli ya mtu mwenye page ya ‘Fans Only’ ambayo ‘followers’ wake wanalipia kumwona akiwa nusu uchi au uchi kabisa?

Alishaniambia mamangu, mwanamke anapokuwa mvivu ataishia kuwa mhanyaji. Huddah anayekesha kuwatusi wanawake wengine kafanikiwa kwa nini haswa? Au ni zile biashara zake ndogo za kuuza lipstiki ambazo nina uhakika katu haziwezi kutosha maisha anayoishi? Sio siri anaishi maisha yake ya kifahari kwa kuuza sura ila kwa kuwatusi wenzake ndio hakosi.

Napenda sana alivyojibiwa na Noti Flow, kwamba kaumwa kwa sababu hakuamini mwanamke ambaye hajafanyiwa upasuaji ili kubadilisha mwonekano wake angeishia kuwa na ‘followers’ wengi kumliko. Hili lina ukweli wake. Kwa nini aumizwe na mafanikio ya mwenzie?

Na labda nikukumbushe tu sio kitambo sana Julai 2017, Huddah alipotimiza ‘followers’ milioni moja, aliposti ujumbe kama wa Tanasha akiwashukuru mashabiki wake. “Thank You for 3M!! Love you guys so much”, ndivyo alivyoandika Tanasha, posti iliyomuuma Huddah kiasi chake kuanza kumshambulia bila sababu. Kwa kuwa yeye ni mbogo, kasahau posti yake ya Julai 2017 baada ya kupata ‘followers’ milioni. “Thanks a million bosses. Thanks for the continued love and support over the years. Be blessed. Thank You. Thank You”, ndivyo alivyoandika Huddah.

Sasa leo kinachomwasha na mwenzake ni nini haswa? Au kwa sababu mwenzake kampitiliza? Huddah haamini kuwa mwanamke anaweza kuwa na ‘followers’ wengi kumliko bila ya kujianika uchi. Hizi darasa za maendeleo anazojifanya kutoa anapaswa kujipa yeye. Tabia hizi ni za mtu anayeteswa na wivu. Huddah bora afanye yake huko Uarabuni alikohamia na amwache mwenzake naye afanye yake!

You can share this post!

KIKOLEZO: Mbwembwe za showbiz

Mfanyabiashara aliuawa kinyama – Uchunguzi