• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 7:55 AM
Trump kuhutubia mkutano akilenga kuwania tena 2024

Trump kuhutubia mkutano akilenga kuwania tena 2024

Na AFP

WASHINGTON D.C., Amerika

ALIYEKUWA rais wa Amerika Donald Trump, Jumapili atarejea katika siasa akitaka kuthibiti chama cha Republican ambacho kiliondoka mamlakani na kuwazia iwapo anaweza kushinda tena kwenye uchaguzi wa 2024.

Baada ya kushindwa kuthibiti seneti, urais na bunge la wawakilishi, vyama vya kisiasa nchini Amerika kwa kawaida huwa vinajipanga upya, kumsahau kiongozi aliyeshindwa.

Lakini Trump angali maarufu katika chama cha Republican na macho yote yatakuwa kwa mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 74 atakapohutubia kongamano la Conservative Political Action Conference na kudokeza kuhusu mipango yake ya kisiasa siku zijazo.

Atahutubu siku ya mwisho ya kongamano hilo ambalo linafanyika Orlando, Florida na anatarajiwa kupokewa kwa shangwe na wanachama wa vyama vya kisiasa visivyotaka mageuzi Amerika.

Lakini je, angali kiongozi wa chama hicho licha ya kushindwa na Joe Biden? Au Trump amekuwa yule ambaye aliondoka Washington kwa aibu, akapigwa marufuku Twitter na kulaumiwa kwa kuchochea uvamizi katika majengo ya bunge?

Ingawa Trump ametulia katika boma la Mar-a-Lago jimbo la Florida, baada ya kutumia miezi kadhaa, alisambaza madai ya uongo kwamba uchaguzi ulikuwa na wizi wa kura, wanamikakati ya wabunge wengi wanasema kwamba angali na ushawishi wa kisiasa katika chama chake.

“Trump ndiye kiongozi wa chama cha Republican,” mbunge Jim Jordan alitangaza kwenye Twitter mnamo Jumatano.

Duru zinazofahamu mipango ya Trump zinasema kwamba rais huyo wa zamani atazungumzia kuhusu hali ya baadaye ya chama cha Republican kwenye hotuba yake katika kongamano hilo na atakosoa baadhi ya sera mpya za Biden.

Lakini huenda asitangaze mipango yake kuhusu 2024 katika kongamano hilo lililoanza Ijumaa.

Mwandalizi wa kongamano, Matt Schlapp, ambaye ni mtetezi sugu wa Trump aliandika kwenye Twitter kwamba rais huyo hatatangaza azma yake ya urais 2024 lakini atachangamkia wazo hilo.

Wanaomezea tiketi ya urais ya chama hicho akiwemo aliyekuwa waziri wa mashauri ya kigeni Mike Pompeo, Gavana wa jimbo la South Dakota Kristi Noem na seneta Josh Hawley watahutubia kongamano hilo.

Utafiti uliofanywa kati kati ya Februari ulionyesha kuwa wafuasi watatu kati ya wanne wa chama cha Republican wanataka Trump atekeleze jukumu muhimu chamani.

Taharuki kuhusu Trump iliongezeka Jumatano kwenye mkutano wa maafisa wa chama hicho na wanahabari. Alipoulizwa iwapo Trump anafaa kuhutubia kongamano, kiongozi wa wachache katika congress Kevin McCarthy alisema “ndio, anafaa.”

Liz Cheney mbunge wa chama hicho aliyeunga mswada wa kumtimua Trump alisema ni juu ya kongamano kuamua akisema kwamba kufuatia uvamizi wa wafuasi wake katika majengo ya bunge Januari 6, haamini iwapo Trump anafaa kutekeleza jukumu lolote katika chama au nchi.

You can share this post!

Sihitaji BBI kuingia Ikulu, Raila asisitiza

MUTUA: Serikali isithubutu kutoza ushuru raia walio...