• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
Wakazi sasa kusafisha jiji kila mwezi

Wakazi sasa kusafisha jiji kila mwezi

Na WACHIRA MWANGI

WAKAZI wa Kaunti ya Mombasa wametakiwa kujitwika jukumu la kuhakikisha jiji hilo ni safi kila mara kwa kujizuia kutupa taka ovyo ovyo na pia kusafisha maeneo wanakofanyia biashara na kuishi.

Idara ya mazingira, kawi na uzoaji taka katika kaunti hiyo Jumamosi ilianzisha rasmi shughuli za kusafisha mji huo, shughuli ambayo itakuwa ikiendelea kila Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi.

Afisa Mkuu wa Kaunti, Ilhan Abass alisema shughuli hiyo itahakikisha kuwa jiji hilo linakuwa safi na pia kuwazoesha wakazi kutupa takataka katika maeneo yaliyotengewa uchafu huo pekee. Bi Abass aliyekuwa akizungumza alipozuru jaa la takala VOK katika eneobunge la Nyali, aliwataka wakazi wajizoe kudumisha usafi badala ya kuachia usimamizi wa Kaunti kazi hiyo.

“Tuko hapa kuanzisha rasmi shughuli ya kusafisha jiji letu ambayo itakuwa ikifanyika siku moja kila mwezi. Shughuli hii inaendelea katika maeneobunge yote sita. Wananchi wajue takataka zote zinazolewa maeneo yanayotambulika na kila mmoja afaa atimize viwango vya juu vya usafi badala ya kuona jukumu hilo kama la kaunti,” akasema Bi Abass.

“Wakazi nao pia wanafaa wajitokeze kushiriki shughuli hii kila mwezi ili iwe tamaduni ambayo itahakikisha jiji letu linarejelea usafi wa viwango vya juu kama zamani,” akaongeza.

Naye mwenyekiti wa Shirika la Msalaba Mwekundu tawi la Mombasa, Bw Mahmoud Noor ambaye alikuwa kati ya walioshiriki usafi huo, aliwataka raia washirikiane na Kaunti na pia wajizuie kutupa taka kiholela maeneo yasiyotengewa uchafu.

“Tunachukua fursa hii kusaidia Kaunti kutekeleza usafi jijini na mitaa mbalimbali. Wakazi wa Mombasa wanafaa wafahamu kuwa jukumu kubwa la kuzingatia usafi linaanza nao wala si serikali. Kila mmoja awajibike kwa kutupa taka eneo linalofaa,” akasema Bw Noor.

Pia aliwataka wazazi wawafundishe watoto wao njia ya kudumisha usafi na umuhimu wa kuishi katika mazingira safi. Tayari Kaunti imefanya hamasisho kuhusu shughuli hiyo kwa wakazi wake na wale ambao watapatikana wakitupa taka ovyo ovyo watachukuliwa hatua kali kulingana na sheria.

“Mtu atakayepatikana akitupa takataka mahala popote na kuchafua mazingira atakabiliwa kisheria.”

Mara hii hatutakuwa na huruma na watalazimika kulipa faini ya Sh500,000. Tunataka jamii ambayo ina ustaarabu na inawajibikia usafi wa mazingira,” akaonya Bi Abass.

Afisa huyo aliwataka wasimamizi wa wadi na wazee wa vijiji wapige ripoti kuhusu wale wanaokiuka sheria za kudumisha usafi.

Mnamo Februari, kaunti ya Mombasa ilianza kutekeleza sheria ya kuwatoza faini ya Sh500,00 kwa wale wanaotupa takataka maeneo yasiyofaa kama njia ya kukabiliana na tabia hiyo inayolemaza usafi wa jiji la Mombasa.

Pia kaunti imewaajiri wafanyakazi 4,000 wa kuzoa takataka pamoja na kununua magari ya kusafirisha takataka hadi jaa la

You can share this post!

Biashara ya mkojo wa wajawazito yanoga TZ

Uhuru huenda apanga kumkweza Gideon kisiasa kurudisha mkono