• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
‘Red Devils’ wa zamani wanavyoisaidia Inter

‘Red Devils’ wa zamani wanavyoisaidia Inter

Na MASHIRIKA

VIONGOZI wa Ligi Kuu ya Italia (Serie A), Inter Milan, walifungua mwanya wa alama nne kileleni baada ya kuwapiga Genoa 3-0 kwenye mechi iliyowakutanisha Jumapili usiku uwanjani San Siro.

Mabao yote yaliyofumwa wavuni na kikosi cha kocha Antonio Conte kwenye mechi hiyo yalitokana na juhudi za wachezaji wa zamani wa Manchester United.

Romelu Lukaku ambaye pia amewahi kuchezea Chelsea na Everton, aliwafungulia Inter ukurasa wa mabao alipocheka na nyavu za wageni wao baada ya sekunde 32 pekee. Goli hilo lilikuwa lake la 18 kufikia sasa kwenye kampeni za Serie A muhula huu.

Lukaku alichangia goli la pili lililofungwa na Matteo Darmian katika dakika ya 69 kabla ya Alexis Sanchez kuzamisha kabisa chombo cha Genoa dakika nane baadaye.

Inter kwa sasa wamejizolea jumla ya alama 56 kutokana na mechi 24 zilizopita. AC Milan waliowapiga AS Roma 2-1 walisalia katika nafasi ya pili kwa alama 52, sita zaidi kuliko mabingwa watetezi Juventus pamoja na Atalanta wanaofunga mduara wa nne-bora.

MATOKEO YA SERIE A (Februari 28):

Inter Milan 3-0 Genoa

AS Roma 1-2 AC Milan

Sampdoria 0-2 Atalanta

Crotone 0-2 Cagliari

Udinese 1-0 Fiorentina

Napoli 2-0 Benevento

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

NDONDI: Kenya yasubiria nafasi mbili zaidi Olimpiki

Simeone afungua mwanya wa pointi 5 juu ya jedwali La Liga