• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Simeone afungua mwanya wa pointi 5 juu ya jedwali La Liga

Simeone afungua mwanya wa pointi 5 juu ya jedwali La Liga

Na MASHIRIKA

ATLETICO Madrid sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) kwa pointi tano zaidi kuliko nambari mbili Barcelona baada ya kuwatandika Villarreal 2-0 mnamo Februari 28, 2021.

Chini ya kocha Diego Simeone, Atletico kinalenga kutawazwa mabingwa wa La Liga kwa mara ya kwanza tangu 2013-14.

Wakicheza dhidi ya Villarreal uwanjani De la Ceramica, Atletico waliwekwa uongozini na Alfonso Pedraza aliyejifunga katika dakika ya 25 kabla ya Joao Felix kucheka na nyavu za wenyeji wao kunako dakika ya 69.

Matokeo hayo yaliwasaza Villarreal katika nafasi ya saba kwa alama 37, nne nyuma ya Real Sociedad watakaopepetana na mabingwa watetezi Real Madrid mnamo Machi 1, 2021 uwanjani Alfredo Di Stefano.

Ushindi kwa Real Madrid ya kocha Zinedine Zidane katika mchuano huo utawapa motisha zaidi ya kuwazamisha Atletico watakaokuwa wageni wao kwenye gozi la La Liga mnamo Machi 7, 2021.

Kufikia sasa, Real wanajivunia alama 52, sita zaidi nyuma ya Atletico waliotamba dhidi ya Villarreal siku nne baada ya chombo chao kuzamishwa na Chelsea waliowapiga 1-0 kwenye mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) jijini Bucharest, Romania.

Atletico wanajivunia safu bora zaidi ya ulinzi katika La Liga msimu huu ikizingatiwa kwamba wamefungwa mabao 16 pekee kutokana na mechi 24 zilizopita. Ingawa hivyo, mechi dhidi ya Villarreal ilikuwa yao ya kwanza kutofungwa kutokana na 10 za awali katika mapambano yote.

MATOKEO YA LA LIGA (Februari 28):

Villarreal 0-2 Atletico

Celta Vigo 1-1 Real Valladolid

Cadiz 0-1 Real Betis

Granada 2-1 Elche

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

‘Red Devils’ wa zamani wanavyoisaidia Inter

AC Milan wapepeta AS Roma