• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 11:55 AM
AC Milan wapepeta AS Roma

AC Milan wapepeta AS Roma

Na MASHIRIKA

AC Milan walipunguza pengo la alama kati yao na viongozi Inter Milan hadi pointi nne pekee baada ya kupepeta AS Roma 2-1 kwenye Ligi Kuu ya Italia (Serie A) mnamo Jumapili usiku.

Franck Kessie aliwaweka Milan uongozini kupitia penalti iliyosababishwa na Federico Fazio wa Roma aliyemchezea Davide Calabria visivyo mwishoni mwa kipindi cha kwanza.

Hata hivyo, Roma walisawazishiwa na Jordan Veretout katika dakika ya 50 kabla ya Milan kufungiwa goli la ushindi dakika nane baadaye kupitia kwa Ante Rebic.

Pigo zaidi kwa Milan ya kocha Stefano Pioli wa Milan ni jeraha la paja lililomweka fowadi veteran Zlatan Ibrahimovic katika ulazima wa kuondolewa uwanjani katika kipindi cha pili.

Milan wamepangiwa kuchuana na Manchester United kwneye hatua ya 16-bora ya Europa League mnamo Machi 11 na 18, 2021. Ni mechi ambazo zinatarajiwa kumkutanisha Ibrahimovic, 39, na waajiri wa zamani waliojivunia huduma zake kati ya 2016 na 2018 ugani Old Trafford.

Ibrahimovic amefungia Milan jumla ya mabao 14 kutokana na mechi 24 za hadi kufikia sasa kwenye Serie A msimu huu.

Milan ambao kwa sasa ni wa pili jedwalini kwa alama 52, walishuka dimbani kuvaana na Roma wakilenga kusajili ushindi wa kwanza baada ya mechi nne za awali katika mashindano yote. Kikosi hicho cha kocha Pioli kinafukuzia taji la kwanza la Serie A tangu 2010-11.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Simeone afungua mwanya wa pointi 5 juu ya jedwali La Liga

Wamiliki wa Inter Milan wafunga kikosi cha Jiangsu FC