• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 6:50 PM
Serikali yaahidi kulinda chanjo ya corona dhidi ya matapeli

Serikali yaahidi kulinda chanjo ya corona dhidi ya matapeli

NA ELIZABETH MERAB

SERIKALI imeeka mikakati ya kuzuia wizi wa chanjo za kukinga virusi vya corona ambazo zinatarajiwa kuingia nchini leo usiku.

Waziri wa Afya, Bw Mutahi Kagwe, alisema Jumapili kwamba maandalizi yamekamilika kupokea chanjo hizo wiki hii. Imefichuka kuwa, baadhi ya wadau katika sekta ya afya wamekuwa na wasiwasi kwamba huenda kuna wafanyabiashara laghai wanaosubiri chanjo hizo kwa hamu, ili watumie utapeli kuzipata na kuuza kwingine.

Hofu hiyo imesababishwa na jinsi ambavyo vifaa vya kupambana na corona viliingiwa doa la ufisadi, kiasi kwamba baadhi ya vifaa vya serikali vilidaiwa kupatikana nchi za nje.

Kulingana na Mkuu wa Jopokazi la Kushauri Serikali kuhusu Covid-19, Dkt Willis Akhwale, kila chupa ya chanjo itakuwa na alama itakayowezesha serikali kuifuatilia inaposafirishwa.

Alama hiyo pia itatumiwa kuthibitisha ni mali ya serikali.Mzigo huo muhimu unatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA), kisha shughuli ya kuthibitisha mzigo mzima ifanywe ndiposa usafirishwe hadi eneo la hifadhi.

 

You can share this post!

Wahudumu wa tuktuk Githurai wahimizwa kushirikiana

Chaguzi ndogo kuamua vigogo wa siasa Magharibi