• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Makamu wa Rais Zimbabwe ajiuzulu kuhusu video ya ngono

Makamu wa Rais Zimbabwe ajiuzulu kuhusu video ya ngono

Na AFP

Tafsiri: Charles Wasonga

HARARE, Zimbabwe

MAKAMU wa Rais wa Zimbabwe Kembo Mohadi alijiuzulu Jumatatu kwa kuhusishwa na tuhuma za uhalifu wa kingono, tukio ambayo ni nadra kuchukuliwa na afisa wa umma katika taifa hilo.

Tangu mwezi jana vyombo vikuu vya habari vilisambaza kanda ya sauti kuhusu mazungumzo ya simu ambapo inadaiwa kuwa Mohadi alikuwa akiwatongoza wanawake walioolewa. Miongoni mwa wanawake hao ni mfanyakazi wa cheo cha chini katika afisi yake.

Kanda hiyo ya sauti ilisambazwa kwa mara ya kwanza ni gazeti la mtandao la ZimLive. Katika kanda hiyo, mwanamume anasikika atoa miadi ya ngono afisini mwake.

“Najiondoa kama Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe… mara moja,” akasema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71, katika barua iliyochapishwa katika akaunti ya twitter ya Wizara ya Habari.

Alieleza kuwa ajiondoi “kwa sababu ya kuwa mwoga,” lakini kwa sababu ya kuheshimu hadhi ya afisini.

“Namechukua hatua hii ili afisi hii ilikoseshwe heshima na madai ambayo yamehusishwa changamoto zinazonikabili kama mtu binafsi,” Bw Mohadi akasema.

“Nimekuwa nikijisaili kwa muda mrefu lakini sasa nimeamua kwamba nahitaji nafasi ya kukabiliana na matatizo yangu nje ya serikali,” akaongeza.

Hata hivyo, Bw Mohadi alikana kuhusika katika uovu huo akisema ameelekezewa madai hayo yasiyo na ukweli na mahasidi wake wa kisiasa. Alisema ataelekea kortini kuvishtaki vyombo vya habari vilivyosambaza madai hayo.

Kujiuzulu kwa Makamu huyo wa Rais kumechochea msisimko mkubwa katika mitandao ya kijamii huku Rais Emmerson Mnangagwa akielekezewa macho kuhusu ni nani atamteua kuchukua mahala pa Bw Mohadi.

Mwanasiasa huyo ni mwanajeshi mstaafu na mmoja wa wapiganiaji uhuru wa Zimbabwe. Ni mmoja wa makamu wawili wa rais nchini humo pamoja na Bw Constantino Chiwenga.

Mohadi alihudumu katika nyadhifa mbalimbali za uwaziri chini ya utawala wa rais wa zamani Robert Mugabe. Aliteuliwa kuwa Makamu wa Rais mnamo 2017 baada ya kung’olewa mamlakani kwa marehemu Mugabe.

You can share this post!

Mihemuko kuhusu video ya utani Pakistan

Waliomuua msichana 9, wakimtoa mapepo wakamatwa