• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 1:08 PM
Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko atimuliwa kwa ubakaji Senegal

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko atimuliwa kwa ubakaji Senegal

Na AFP

DAKAR, Senegal

KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko amesema atajiwasilisha mahakamani Jumatano kujibu madai ya kushiriki ubakaji.

Mwanasiasa huyo amekuwa akizingirwa na lawama tangu mwezi jana wakati vyombo vya habari nchini Senegal viliripoti kwa mhudumu katika saluni moja ambako alienda kukandwa misuli (massage) alimshtaki mwa kumdhulumu kimapenzi.

Sonko, ambaye ni kiongozi wa chama kinachojulikana kama, Pastef Party, hata hivyo amekana madai dhidi yake huku akimsuta Rais wa Senegal Macky Sall kwa kuendeleza njama ya kumwondoa mamlakani kabla ya uchaguzi wa 2024.

Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 46, alishindana na Rais Sall katika uchaguzi muu wa 2019 lakini akawa nambari tatu, katika kinyang’anyiro hicho kilichomwezesha rais huyo kuhudumu muhula wa pili.

Sonko aliwaambia wanahabari Jumanne usiku kuwa atatii agizo la kufika mahakamani Jumatano katika atashikilia kuwa hana kosa.

“Tutafika mbele ya jaji lakini nitasisitiza kuwa sina sikushiriki uhalifu huo,” akasema akikariri madai dhidi ya Rais Sall.

Mwanasiasa huyo aliagizwa kufika kortini baada ya Bunge la Senegal wiki jana kupitisha hoja ya kumpokonya kinga dhidi ya mashtaka. Hatua hiyo ilitoa nafasi kwa polisi kuendesha uchunguzi kuhusu madai dhidi yake.

Mwezi jana mamia ya wafuasi wa upinzani walifurika barabarani wakimtetea Sonko, hatua ambayo ilisababisha makabiliano makali dhidi yao na polisi.

Madai ya ubakaji dhidi ya Sonko huku kukiwa na tashwishi ikiwa Sall, 59, atagombea urais kusaka muhula wa tatu uongozi.

Marais nchini Senegal huhudumu kwa mihula miwili pekee, lakini Rais Sall alishinikiza mabadiliko ya Katiba mnamo 2016 yaliyochangia kuondolewa kwa hitaji hilo. Hatua hiyo ilisababisha kuwepo kwa uvumi kwamba anapania kuwania urais mara tatu.

Marais wengine katika mataifa ya Afrika Magharibi kama Alpha Conde wa Guinea na Alassane Ouattara wa Ivory Coast wamewahi kushinikiza mabadiliko ya Katiba ili kuweza kusalia mamlakani.

 

Tafsiri: CHARLES WASONGA

You can share this post!

Kupata chanjo hakumaanishi mlegeze masharti ya Covid-19 ...

Lazio watia kapuni alama tatu za bwerere Serie A baada ya...