• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 12:32 PM
Echesa akamatwe – Mutyambai

Echesa akamatwe – Mutyambai

NA LEONARD ONYANGO

Inspekta Jenerali wa Polisi Hillary Mutyambai ameagiza waziri wa zamani wa Michezo Rashid Echesa akamatwe mara moja kwa kuwa “sasa ni mhalifu hatari.”

Bw Mutyambai aliagiza maafisa wa usalama wamsake na kumsukuma ndani Bw Echesa baada ya kukataa kujisalimisha kufikia Ijumaa saa saba mchana.

Bw Echesa ambaye ni mwandani wa Naibu wa Rais William Ruto aliingia mitini Alhamisi baada ya kutenda kosa la kumzaba kofi afisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) wakati wa kura za uchaguzi mdogo wa ubunge katika eneobunge la Matungu.

Mara baada ya video inayoonyesha akimtandika kofi afisa wa IEBC kuenea, maafisa wa polisi walizingira nyumba yake lakini hakiwepo.

“Echesa alistahili kujisalimisha katika kituo chochote cha polisi kufikia saa saba mchana. Akikosa kujisalimisha, na atachukuliwa kuwa mhalifu hatari aliye na silaha,” akasema Bw Mutyambai.

Pia aliagiza maafisa wa polisi kuwafikisha mahakamani wanasiasa waliokamatwa kwa fujo katika maeneo mbalimbali ambapo kulikuwa na uchaguzi mdogo Alhamisi.

You can share this post!

Barasa: Waliozua fujo Kabuchai wangali huru, tunaonewa kama...

Ni kubaya 2022!