• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 9:55 AM
Mwatate yajiandaa kuonyesha ubabe wake Kisumu Jumatatu

Mwatate yajiandaa kuonyesha ubabe wake Kisumu Jumatatu

Wachezaji wa Mwatate United FC wakipasha misuli kabla ya mechi yao ya nyumbani dhidi ya Sony Sugar FC iliyofanyika uwanja wa Dawson Mwanyumba mjini Wundanyi, Februari 13, 2021. Picha/Abdulrahman Sheriff

NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MWATATE United FC imeondoka kuelekea Kisumu ambako imepangiwa kupambana na Kisumu All Stars FC kwenye mechi ya Supaligi ya Taifa itakayochezwa Jumatatu Machi 8 katika uwanja wa Moi kuanzia saa tisa alasiri.

Kocha Mkuu wa timu ya Mwatate United FC, Andrew Kanuli aliambia Taifa Dijitali kuwa wamejiandaa vya kutosha na hana tatizo la majeruhi hivyo wana tamaa kubwa ya kurudi na pointi zote tatu kutoka Kisumu.

“Tunahitaji kuhakikisha tumerudi na alama zote tatu kwa sababu tunahitaji kupanda ngazi. Tumekuwa tukiendelea kufanya vizuri na tunataka kuhakikisha tunakuwa karibu ili tupate morali ya kuwapiku wale walioko juu yetu,” akasema Kanuli.

Mwenyekiti wa klabu hiyo, James Okoyo anasema kuwa wameondoka na wanatarajia kuwasili Kisumu Jumamosi usiku ili asubuhi ya Jumapili wapashe misuli wakisuri siku ya mechi itakayochezwa Jumatatu.

“Nina matumaini makubwa wachezaji wetu walivyo na morali, tunawaambia wafuasi wetu waiombee timu Mungu iweze kufika salama na kucheza na kuweza kupata ushindi,” akasema Okoyo.

Mwatate United iko nafasi ya sita na ikishinda inaweza kupanda hadi kuwabandua wenzao wa jimbo la Pwani, Coast Stima kwenye nafasi ya tatu lakini hilo itategemea kama timu zilizo juu ya Mwatate zitapoteza nafasi zao.

You can share this post!

Musiala atia saini kandarasi ya kuchezea Bayern hadi 2026

Nzoia, Bandari Zagawana Pointi Kwenye Mechi ya Ligi Kuu