• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 9:50 AM
FUNGUKA: ‘Si uchizi, ni raha zangu…’

FUNGUKA: ‘Si uchizi, ni raha zangu…’

Na PAULINE ONGAJI

HIVI majuzi nilipata fursa ya kukutana na binti mmoja kwa jina Mercy.

Binti huyu mwenye umri wa miaka 45 hajawahi olewa wala kuwa na watoto licha ya kuwa mrembo ajabu na kutaalumika vilivyo.

Tumfahamu Mercy kwanza. Ameajiriwa katika mojawapo ya kampuni kuu za kimataifa kama mkuu wa masuala ya mawasiliano na mahusiano. Taaluma yake ya hali ya juu ina mshahara mkubwa, na hivyo imemruhusu kumiliki jumba kubwa la kifahari na baadhi ya magari ya bei ghali.

Kimaumbile, Mercy ameneemeka kutoka utosini hadi miguuni. Yeye ni mrembo sana. Sura yake ya kupendeza huwaacha wengi wanaokutana naye wakidondokwa na mate, huku akiandamwa na madume kutoka kila pembe ya dunia.

Lakini licha ya sifa hizi, binti huyu hana haja na masuala ya mahusiano. Mara yake ya mwisho kuwa na mchumba wa kudumu ilikuwa miaka 20 iliyopita. Hii ni licha ya kukutana na madume wanaotaka kumchumbia kila wakati.

Uamuzi wake wa kutoolewa wala kutopata watoto ni wa hiari na ana sababu za kustaajabisha.

“Kwanza kabisa, mahitaji yangu ya mahaba, kwa kiwango fulani huridhishwa kwa kutazama wanaume wanaoshamiri kimaisha. Nafurahia kumuona mwanamume akijiendeleza kimaisha, ambapo kiu yangu ya mahaba inashibishwa ninapomfadhili kaka huyu kwenda shuleni au katika miradi yake.

Pili, tangu utotoni hamu ya mahaba haijawahi tawala hisia zangu, na hivyo masuala ya tendo la ndoa hayanivutii. Badala yake namtaka mwanamume awe tayari kunipa pambaja tu na kunipapasa.

Tatu, ninapolemewa sana na kiu ya mahaba, haja zangu hutimizwa kupitia njia zisizo za kawaida. Tukiingia chumbani naridhishwa ninapomuona kaka akiwa nadhifu kwa kudumisha usafi, kuvalia suti kila mara na kujipulizia marashi miongoni mwa mambo mengine kabla ya kunifunga kwa kamba na kunicharaza kwa mjeledi.

Najua wengi wanadhani kuwa mimi ni wazimu lakini sio hivyo. Napata raha kwa kusikia maumivu na hasa kwa uchungu wa mjeledi mgongoni. Hisia za maumivu hunichangamsha.

Lakini katika haya yote, kaka anayenihudumia anapaswa kuelewa kwamba sitaki mwunganisho wowote wa kudumu naye.

Kwa upande wangu niko tayari kumfanyia chochote atakayekubali maisha haya, ikiwa ni pamoja na kumnunulia jumba la kifahari, gari na hata kugharimia mahitaji yake ya kifedha.

Miongoni wa wanaume wanaopata fursa ya kuonja maisha haya, wengi hutaka kurejea na kutaka kuendeleza uhusiano nami ila sina haja. Wengi wamejaribu kunibembeleza na hata kunipigia magoti lakini nimekata kauli na kamwe sitawahi legeza kamba.

Kuna watu wanaodhani kuwa mimi ni chizi lakini sivyo. Ukweli ni kuwa mimi ni tofauti, na masuala ya kawaida ya mahaba hunichosha”.

You can share this post!

KAMAU: Serikali isaidie HELB kutoa mikopo upesi kwa...

CHOCHEO: Ukijua anachepuka, utafanyaje?