• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 8:55 PM
Korti yakataa kutupa kesi ya mauaji dhidi ya Babu Owino

Korti yakataa kutupa kesi ya mauaji dhidi ya Babu Owino

Na RICHARD MUNGUTI

MBUNGE wa Embakasi Mashariki Bw Paul Ongili almaarufu Babu Owino jana alipata pigo wakati mahakama ilipokataa kutamatisha kesi inayomkabili ya kujaribu kumuua Bw Felix Orinda almaarufu DJ Evolve.

Hakimu Mwandamizi wa mahakama ya Milimani, Bw Bernard Ochoi, alisema hakuna ushahidi wa kuridhisha kuonyesha kwamba mlalamishi amefidiwa.

Mbunge huyo alidaiwa kujaribu kumuua Bw Orinda kwa kumpiga risasi wakiwa katika kilabu moja iliyoko eneo la Kilimani, jijini Nairobi.

Alipowasilisha ombi mbele ya Bw Ochoi kutaka kesi itamatishwe, Bw Owino alidai kuwa wamekubaliana na familia ya mhasiriwa kwamba aendelee kugharimia matibabu yake katika Nairobi Hospital alikolazwa.

Hata hivyo, hakimu alisema kwamba mwanasiasa huyo hajawasilisha ushahidi unaoonyesha mkakati alioweka “kurekebisha tabia na maadili yake”.

Bw Orinda alipata majeraha katika uti wa mgongo na anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya Nairobi. Wakati huo huo, mwanawe aliyekuwa Gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu jana alikiri mashtaka ya kuendesha gari akiwa mlevi.

Brian Ndungu Waititu alitozwa faini ya Sh30,000 kwa kuendesha gari aina ya Probox jijini Nairobi akiwa mlevi.Alikiri makosa yake mbele ya hakimu mwandamizi Bi Esther Kimilu kuwa tukio hilo lilitendeka mnamo Machi 15 katika barabara ya Muindi Mbingu iliyo katikati ya jiji.“Naomba msamaha na sitarudia makosa haya tena.

Nionee huruma,” Ndungu aliirai mahakama.Baadaye alisikika akisema kwa simu kwamba baba yake asingemsaidia baada ya kukamatwa kwa sababu tayari alikuwa ashamkanya akome tabia hiyo ya ulevi.

You can share this post!

Mafuta ghali: Wakenya wakerwa na wabunge kujifanya...

Uhuru amwomboleza mwanahabari aliyefariki kutokana na corona