• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
Maeneobunge 70 zaidi ni haramu – Chebukati

Maeneobunge 70 zaidi ni haramu – Chebukati

Na CHARLES WASONGA

TUME Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetaja maeneo bunge mapya 70 yaliyopendekezwa katika Mswada wa marekebisho ya katika kupitia mpango wa maridhiano (BBI) kama haramu.

Akiongea Jumatano alipofika mbele ya kamati ya pamoja ya wabunge na maseneta inayokusanya maoni ya umma kuhusu mswada huo, mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati hatua hiyo ni kinyume cha Katiba kwa sababu hawakuhusishwa.

“IEBC ilipaswa kuhusisha katika taratibu zote za kupendekezwa na kugawanywa kwa maeneo bunge hayo mapya inavyoelezwa katika vipengele vya 84 (4) na 89. Hii ni kwa sababu tume hii ndio yenye mamlaka kikatiba kuamua ni sehemu ambazo zinapaswa kuongezwa maeneo bunge zaidi,” Bw Chebukati akawaambia wanachama wa kamati ya pamoja na seneti na bunge kuhusu sheria, katika majengo ya bunge, Nairobi.

“Akaongeza: “Kubuniwa kwa maeneo bunge mapya kupitia bunge au kura ya maamuzi kunaweza tu kuwa halali ikiwa IEBC itaachiwa kazi ya kuyagawanya katika kaunti mbalimbali. Kwa kuwa waandalizi wa mswada wa BBI hawakufanya hivyo, walikiuka Katiba.”

Kulingana na Mswada wa BBI, maeneo bunge hayo mapya yamegawanya kati ya kaunti 28 ambapo kaunti ya Nairobi ikitengewa maeneo bunge 12 zaidi.

You can share this post!

MAFUTA: Wakenya wakimbilia Tanzania

WANDERI KAMAU: Tujuzwe sababu za bei ya mafuta kupanda kila...