• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 11:05 AM
SAMIA SULUHU: Rais mtarajiwa wa Tanzania

SAMIA SULUHU: Rais mtarajiwa wa Tanzania

AGGREY MUTAMBO NA WANGU KANURI

WATANZANIA sasa wapo tayari kuzoea utawala wa kwanza wa rais mwanamke, Makamu wa Rais Samia Suluhu. Hii ni baada ya kifo chake Rais John Pombe Magufuli, mnamo Jumatano. 

Rais Magufuli amefariki akiwa mwenye umri wa miaka 61 na kuacha pengo katika uongozi wa taifa hilo. Hii inamaanisha kuwa Bi Suluhu, aliye na umri wa miaka 62, atatarajiwa kumiliki ofisi ya juu sana nchini humo kulingana na sheria za taifa hilo.

Kifungu 37 cha Katiba ya Tanzania kinasema kuwa makamu wa rais anauchukua usukani wa uongozi kwa kipindi kilichosalia na atastahiki kuwa mgombeaji wa kiti hicho katika uchaguzi ujao. Hali kadhalika, nchini Tanzania hakuna shaka kuhusu urithi lakini kuwa na rais mgonjwa kuliwapa mtanziko mpya.

Kwa wiki nyingi, wakuu katika serikali hiyo walikataa uvumi wa kuwa na rais asiyejiweza lakini wakashindwa kumuonyesha kwa umma uliokuwa ukisubiri kwa hamu. Kifo chake kinatuliza uvumi uliokuwa ukienea. Lakini sasa urithi wa uongozi.

Ikiwa atauchukua uongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi Suluhu atakuwa mwanamke wa pili katika Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa rais. Atakuwa Mzanzibari wa kwanza tangu Ali Hassan Mwinyi kuongoza Jamhuri ya Muungano.

Hata hivyo sheria iyo hiyo ya Tanzania inasema kuwa rais akiwa mgonjwa haimaanishi kuwa kiti cha rais ki wazi.

Isitoshe, Bi Suluhu, ndiye mwanamke wa pili kama makamu wa rais katika Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya makamu wa rais wa Uganda Specioza Kazibwe. Akiwa mwenye umri wa miaka 61, mheshimiwa Kazibwe ndiye makamu wa rais wa kumi katika taifa hilo.

Kazi yake katika siasa ilianzia Zanzibar ambako alihudumu katika baraza la mawaziri. Bi Suluhu, kiongozi alisomea katika nchi ya Tanzania, India, Pakistan na Amerika, amekuwa uso wa Tanzania katika hafla za bara huku mara nyingi akisafiri kwa niaba ya rais Magufuli ambaye alitoka nje ya Tanzania kinadra sana.

Chini ya Rais Kikwete, Bi Suluhu alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Muungano kati ya Tanzania na Zanzibar.

Lakini je, anaweza kupanda madarakani ipasavyo?

Bw Magufuli ambaye alipewa jina la lakabu ‘Bulldozer’ kwa kusukuma miradi alipokuwa akifanya kazi katika Wizara ya Kazi, alikuwa akisema kuwa angeondoka baada ya kipindi chake cha uongozi kutamatika huku akiashiria kupokezana uongozi kwa atakayemrithi.

Lakini baadhi ya wachambuzi wa kisiasa nchini Tanzania walisema kuwa mpango ulinuia mwanawe Mwinyi, mtoto wa rais wa nchi ya Zanzibar Hussein Mwinyi, kuuchukua uongozi huo.

“Iwapo Bi Suluhu atauchukua usukani wa serikali, ataonyesha mpango wa kurithiana kisiasa. Sheria iko upande wake, lakini hivi sasa atahitajika kung’ang’ana ili akubalike,” alisema mwanasayansi wa mambo ya kisiasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye alizungumza nasi kwa njia ya siri kwa sababu ya kuhofia usalama wake.

“Ni kweli kuwa Bw Magufuli amekuwa na uhusiano mzuri wa kikazi na Mwinyi. Alimteua Magufuli kama Waziri wa Mambo ya Ndani katika kipindi chake cha kwanza cha uongozi na akaidhinisha ugombezi wake nchini Zanzibar,” mtaalamu huyo akaongeza.

Bw Magufuli na mgombezi mwenzake Bi Samia Suluhu, aliwania kiti cha urais kupitia chama cha CCM na akawashukuru mabalozi wa chama cha bunge la kitaifa, jijini Dodoma mwaka wa 2015.

Chama cha CCM kinajulikana katika nchi hiyo ya Tanzania na nchi ya Zanzibar na chama hicho kimekuwa kwenye uongozi tangu uhuru (japo CCM yenyewe ilibuniwa baada ya muungano kati ya Tanganyika African National Union TANU na chama cha Zanzibar Afro-Shirazi mnamo mwaka wa 1977.

Fauka ya shutuma kutoka wapinzani wa vyama vingi, chama cha CCM kimeweza kuimudu misukosuko hii, huku ikijishindia viti 262 kati ya viti 264 vya bunge mwaka jana.

“Chini ya sheria, Makamu wa Rais anatamatisha kipindi cha uongozi wa rais iwapo rais huyo hatakuwa na uwezo. Pia anaweza kuwa kwenye kinyang’anyiro cha uongozi wakati wa uchaguzi mkuu na anaweza stahiki kuwa kiongozi hadi mara ya tatu iwapo wakati ambapo aliuchukua uongozi wa urais, uongozi huo ulikuwa chini ya miaka mitatu,” alieleza mwanasheria wa Tanzania.

“Tunatarajia kuwa iwapo atauchukua uongozi sasa, atahitaji kudhibitiwa kwa kazi yake ifikapo mwaka wa 2025. La sivyo, wasomi watatumia ujanja wao na kufanya wanaotaka wawe katika kinyang’anyiro cha urais,” akasema.

Suluhu kama makamu wa rasi anaongoza bunge la kitaifa la chama hicho, kiungo kinachoamua ni nani atapeperusha bendera ya urais.

You can share this post!

Mwalimu taabani kwa kumdhulumu mtahiniwa wa KCSE

Upinzani TZ wataka Mama Samia Suluhu kuapishwa kuwa Rais...