Spika wa Bunge la Tanzania awaita wabunge Dodoma

NA ELIZABETH EDWARD, MWANANCHI

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amewataka wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda bungeni mjini Dodoma.

Ndugai ameeleza hayo leo Alhamisi Machi 18, 2021 ikiwa ni saa kadhaa tangu Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo cha Rais John Magufuli.

“Kama mnavyofahamu waheshimiwa wabunge walikuwa wawe katika ziara za kukagua miradi ya maendeleo kutokana na utekelezaji wa bajeti inayoendelea inayokwisha Juni 30, 2021.”

“Na matarajio yetu ni kwamba waliokuwa waendelee na ukaguzi wa miradi hiyo imebidi tutoe wito na maelekezo kwamba wabunge wote waliokuwa katika ziara hizo za ukaguzi wa maendeleo warudi Dodoma haraka sana,” amesema Ndugai.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Rais Magufuli, zilitangazwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6.

Habari zinazohusiana na hii