• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:30 PM
Utawala wa Magufuli ulikandamiza haki za kibinadamu

Utawala wa Magufuli ulikandamiza haki za kibinadamu

NA LEONARD ONYANGO

UTAWALA wa Rais John Magufuli umekuwa ukikosolewa kwa kunyanyasa wanaharakati, viongozi wa upinzani, watumiaji wa mitandao na vyombo vya habari.

Tangu kuingia mamlakani, serikali ya Magufuli ilifadhili sheria zilizonyima watu uhuru wa kujieleza na kudhibiti mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na wanahabari.

Mapema wiki hii, idara ya polisi ilitangaza vita dhidi ya watumiaji wa mitandao waliokuwa wakisambaza taarifa za kuugua kwa Rais Magufuli.

Tayari watu wanne, akiwemo fundi wa simu katika mtaa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, Charles Majura, 35, walikamatwa kwa kueneza taarifa hizo ambazo sasa zimeibuka kuwa za kweli.

Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, viongozi wa upinzani nchini Tanzania wamekuwa wakitorokea Kenya kutokana na hofu ya kukamatwa.

Aliyekuwa mwaniaji wa urais, Tundu Lissu, alitoroka Tanzania mnamo Novemba mwaka jana kwa kuhofia maisha yake, sawa na aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, aliyetorokea Kenya kabla ya kupata hifadhi Canada.

Mwaka jana, serikali ya Tanzania iliwataka wanahabari wa mashirika ya kigeni kuandamana na mtu aliyeteuliwa na serikali wanapoenda kutafuta habari nchini humo.Serikali pia imefunga mashirika kadhaa ya habari na kukamata.

 

You can share this post!

Samia Suluhu kuchukua usukani Tanzania kwa kipindi...

Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa sita wa Tanzania